10 Aprili 2012 - 19:30

ABNA inatuarifu kuwa:Wizara ya usalama ya jamhuri ya kiislam ya Iran imetangaza imewakamata majasusi kadhaa na kufanikiwa kuvunja ngome na nguvu za majasusi hao, ambao walikuwa wamepanga kufanya mashambulizii hivi karibuni.

   baada ya kukamatwa majasusi hao, ushahidi umeonekana kuwa baadhi ya nchi za Ulaya na  Marekani na waitifaki wao ndio wanao watuma majasusi hao.anuai za siraha na mitambo mingine ya hali ya juu  ya kijasusi  ilikamatwa katika tukio hilo.

yafaa kuashiria kwamba maadui wa maendelea ya serikali ya kiislam ya Iran wamekuwa wakitumia hila mbalimbali kuhakikisha kwamba wanazuia urutubishaji wa nyukilia wa njia ya amani unaofanyika nchini humo.