9 Oktoba 2012 - 14:47

Diamas Msanii na mwimbaji muziki maarufu wa Ufaransa kukubali Uislam, akieleza kuwa fikira na mwenendo mbovu aliokuwanao ndio sababu ya kuingia katika Uislam, na swala na kusoma Quran kulinyoosha mambo yake.

ABNA- Diamas Msanii na mwimbaji muziki maarufu wa Ufaransa siku kadhaa alisambaza kitabu chake na kueleza kuwa nimechagua Uislam na hijabu kuwa vazi langu.

Jina lake ni Milan Gorgiades aliekubali Uislam November 2009 na kuzuiwa mara kadhaa kuingia Chuo Kikuu kwa kuvaa kwake hijabu, na kuwa sababu kila atakapo kuwepo chini ya darubini ya Waandishi wa habari.

Utunzi wa kitabu chake hicho kinacho zungumzia maisha ya bila Baba na kuingia kwake katika muziki na kushirikiana na wanamuziki wa Marekani katika kuimba muziki na kushiriki vipindi vya Televisheni Nchini Ufaransa kuwa kwake maarufu alisema: nilikuwa katika kilele cha mafaanikio ila la ajabu ni kwamba kila siku nilijihisi bado sijakamilika na kuwa na matatizo ya kisaikolojia na kila siku nilikuwa nikirejea kwa Mwanasaikolojia ili ni tibiwe ugonjwa nilokuwa nao, kwa bahati mbaya sikufaanisha hilo, ila tu kuingia kwangu Uislam yoote nilokuwa nikijihisi yalikwisha na kuwa na katika hali njema.

Mama huyo ni mwenye umri wa Miaka 32 na anao Watoto 4 mmoja wao aitwa Mariam, alikubali Uislam katika Kisiwa cha Moris 2009.

Akieleza: Nilipochukua hatua ya kuvaa hijabu na kusaidia mayatima watu wote walishangaa kwa vazi hili na kubalidisha kwangu Dini.