23 Februari 2013 - 20:30

يا أَيُّهَا الَّذينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثيراً مِنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ وَ لا تَجَسَّسُوا وَ لا يَغْتَبْ بَعْضُكُمْ بَعْضاً أَ يُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَنْ يَأْكُلَ لَحْمَ أَخيهِ مَيْتاً فَكَرِهْتُمُوهُ وَ اتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ تَوَّابٌ رَحيم Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu. Quran 49/12

Uhakikia wa ndoa ni mahusinao ya ulimwengu 2 tofauti katika maisha ya watu wawili ambao wanafisa na tabia totauti. Kwa hiyo maisha kama haya lazima asasi na msingi wake uwe ni upendo wa pande zote mbili na usafi wa kiroho.

Miongoni mwa matatizo yaloikabili jamii yetu katika maisha ya ndoa ni shaka na dhana mbaya ambayo kwa sasa ni hatari katika maisha ya kifamilia, kwa hiyo mwamzo wa ndoa huonekana kufahamiana wawili ila mwisho wake ni kuripuka bomu mripuko hatari.

UANGAMIZAJI WA ATHARI YA DHANA MBAYA:

Sababu ya dhana mbaya hutokea hali ya hapa na pale ya kutoelewana wanandoa katika maisha yao kotokana na baadhi ya sababu ndogo ndogo, tunapoangalia kwa kina ndani kwao, hatukuti isipokua mapenzi yalojaa ndani yake migongano ya hapa na pale na kutofahamiana na kutodhihirisha mapenzi hayo baina yao.

Hakika dhana mbaya ni jambo la kwanza linalosababisha kutoelendelea uhusiano mwema katika maisha ya ndoa, na kusababisha maumivu makubwa katika ndoa na kutopatikana na tiba.

VISABABISHI VYA SHAKA

1-Wivu: Hakika wivu ni moja kati ya mambo makubwa ambayo ya sababisha pande mbili kuona na kufikiria mambo ya sio kuwa na uhakika ndani yake na kupelekea upande wa pili kutuhumu upande mwengine.

2- Usiri katika mambo: Mmoja katika ya wanandoa ajihisi kufanyika kazi kiuficho na hali hii kuendelea kila siku na kusababisha shaka, na inapojitokeza hali kama hiyo katika nasfi hubadilika kuwa dhana mbaya na kusababisha mripuko mkali katika maisha ya ndoa.

3- Kujiona na mashindano: Hali hii mara nyingi hujitokeza kwa vijana kuendeleza hali ya utoto bila kujitambua, kila kinachojitokeza katika maisha ya wanandoa kutokana na hali hii kusababisha kushindana katika maisha yao, na kila mwenye kuanza chokochoko kwa mwenzie hujitahidi upande kuandaa njama ya kujibu chokochoko hizo.

4- Ugonjwa: Kila aina ya magonjwa ya kisaikolojia yaweza kua sababu ya kuleta shaka na hali ya wasiwasi kuwa pande mbili, udhaifu wa kifikra au baadhi ya vitu vilivyomtokea(kufumanuwa au kufumania) mmoja kati ya wanandoa na hali hiyo husababisha kutoamini kitu chochote na kuzaa hali ya shaka katika kila kitu.

Na mengiyo yaweza kua sababu na visababishi vya shaka ambavyo havikutajwa.

DHARURA YA KUJIEPUSHA NA DHANA MBAYA

Dhana mbaya ni miongoni mwa sifa za vijana, kushindwa kufahamiana watu wawili katika maisha yao ya kushirikiana, na hakika kushindwa kwa kufahamiana ni ishara kutoonyesha umuhimu wao katika kujiandaa kuhifadhi kizazi chao kijacho kitabia.

NJIA NA TIBA YA DHANA MBAYA

1- Kujihifadhi: Kila mmoja katika wanandoa wapo sawa katika kutekeleza sheria ya Mwenyezi Mungu hakuna mbora kuliko mwengine, na ni juu yao kujitenga mbali na mambo yanayosababisha  hitilafiu baina yao, kama kumtuhumu mwengine na dhana mbaya.

2- Kuzingatia mipaka ya kibinadamu: Hakika maisha ya ndoa ya maanisha kukusanyika watu wawili kuwa kitu kimoja na kukubalia kuishi katika sakafu moja, na ni juu yao hao watu wawili kuzingatia mipaka ya kibinadamu nayo ni heshima baina ya pande mbili, zingatia kwani heshima ndio ngao ya kila mwanandoa katika ndoa yake.

3- Kujizatiti katika mambo: Hakika kila jambo unalotaka kufanya au kulitolea maamuzi lazima kulifikiria kiundani zaidi kutokana na uchukuaji haraka wa maamuzi huleta nadama babae, kwa mantiki hii kila kitu usichuwe uwamuzi wa haraka haraka kabla ya kutafakari katika jambo.  

4- Kufikiria mambo: Jitahidi kila siku kuwa mwendeshaji na mfikiri wa mambo ya familia yako kwani hakuna mushkili na tatizo chini ya jua, la muhimu ni kwamba kuhukumu mambo kwa akili na kwa huruma na kufiria katika kila nyanja ya maudhui na tatizo na kujitenga mbali na kujiona wewe ndio wewe la hasha usiwe hivyo, kama huwezi kufanya hivyo tafuta mtu mmoja katika jamii awe mshauri wako bila kuangalia miaka na hali ya kijamii.

5- Jujijenga kinafsi: Kila siku mwanadamu ajiweke kuwa ni mwenye kukosea na kutokua mkalifu, kuwa na taswira hiyo ni kujikinga na ubinafsi katika maisha ya ndoa na kuwa taswira hiyo mwanga wa maisha na kukupelekea kwenye ukweli wa mambo.

6- Kukubali ukweli pamoja: Maisha ya kushirikiana lazima yaongozwe na akili zaidi kuliko moyo kadri itakavyo wezekana, kujadili baadhi ya mambo ya kweli pamoja na kuyakubali wote kwa pamoja, na hii yahitaji pande mbili kuaminiana katika mambo na kuwa sawa na kanuni za kifikra.

7- Nia nzuri: Miongoni mwa mambo muhimu katika maisha ya ndoa ni kuwa daima wanandoa na nia nzuri katika maisha yao ya kushirikiana, na kama hawatofanya hivyo basi maisha yao yatageuka kua ni zilzala ya hapa na pale na kutokua na amani ndani ya nyumba yao ambayo watarajia kuleta matuta mema yatakayoongoza jamii.

8- Kukubaliana masharti: Nyinyi si watoto tena ambao mlikua huru hapo jana, hakika maisha ya ndoa ni mingoni mwa aina za uhuru wa kufungwa na masharti, masharti hayo hukubaliana wanandoa kuwa ndio asasi na msingi wa ndoa yao na maisha ya kushirikiana, aidha kuwa maisha hayo ni sharti ya kushirikiana katika maisha ya ndoa ni kwamba masharti hayo huifadhi watu (wanandoa) kitabia na jinsi ya kuishi na kuongea pamoja katika zile kanuni na masharti ambayo mwanzo wake huwa mgumu ila mwisho wake ni maslahi yao ya baadae kuishi wanandoa maisha matulivu bila mzozano wa hapa na pale.

Ndugu mpendwa baada ya kufahamu mambo haya jitahidi kuwa wazi na mshiriki wa maisha yako, fahamu kua matatizo ulokuwa nayo si yako tu bali jamii nzima  imekumbwa na kukabiliwa na matatizo hayo, kwanza kabisa jitahi kumcha Mola wako alokuumba na kumshukuru kila siku kukupa afya njema kwani ni wengi wahitaji kuwa na afya kama yako hawakufaanikiwa hatimae ni kuaga dunia hii dhalili isokua na faida yoyote kwa mwanadamu, dunia hii ni soko hufaidika baadhi na hupata khasara baadhi, daima mwanadamu atarajia kila siku awe mwenye kufaidika, zingatia faida hii tunayotaja hapa si ya siku mbili, mwaka mmoja, miaka ishirini, miaka khamsini au umri wa mwanadamu la hasha ni faida ya baada ya ulimwengu huu wa dunia baada ya kuaga kwetu dunia yaani maisha ya akhera peponi maisha ya milele, kwa mantiki hii lengo la wanandoa si kuishi hapa duniani tu hapana maisha haya ni maandalizi ya maisha ya hapo baadae maisha ya peponi kuwa pamoja peponi kama tulivyokuwa hapa dunia, kwa hiyo kujitahidi kurekebisha matatizo ya ndoa zetu ni kuandaa na kutatua matatizo ambayo yaweza kuwa kiziwizi cha kutupeleka pamoja peponi na kuendeleza maisha yetu ya kushirikiana.

Ndugu wapendwa sote tushikane mikono kusaidizana kupeleka gurudumu hili mbele, kwa kua lengo letu sote moja hakuna kiziwizi cha kutuzuiya kusaidizana na kushikana mikono.