5 Mei 2025 - 23:30
Source: Parstoday
Kukabiliana mataifa ya Amerika Kusini na vita vya ushuru vya Trump

Wanachama wa Soko la Pamoja la Amerika Kusini (Mercado Común del Sur) wameongeza idadi ya bidhaa zisizo na ushuru kwa bidhaa zinazoangizwa kutoka nje ya jumuiya ya kikanda, katika hatua muhimu dhidi ya vita vya kibiashara vilivyoanzishwa na Rais wa Marekani Donald Trump.

Mercosur ni makubaliano ya kibiashara ya kikanda yaliyoanzishwa mwaka wa 1991 na Mkataba wa Asuncion kati ya Brazili, Argentina, Uruguay na Paraguay. Madhumuni yaliyobainishwa ya kuanzishwa kwa Mercosur ni kukuza biashara huria na ubadilishanaji huria wa bidhaa, rasilimali watu na sarafu kati ya nchi wanachama.

Baadaye, Bolivia na Venezuela zilijiunga nayo. Lakini uanachama wa Venezuela umesitishwa. Chile, Colombia, Ecuador, Peru, Guyana, Suriname na Panama sasa ni wanachama muhimu wa Mercosur, huku Mexico na New Zealand zikiwa wanachama waangalizi wa shirika hili la kieneo.

Wanachama wa Mercosur walikutana kwa mara ya pili katika kipindi cha mwezi mmoja katika mji mkuu wa Argentina Buenos Aires na, katika taarifa yao, walisisitiza "makubaliano yaliyofikiwa" juu ya haja ya "kupanua kwa muda" orodha ya kitaifa ya vighairi kwenye Ushuru wa Pamoja wa Nje (AEC) wa kila nchi mwanachama.

Ili kuimarisha unyumbulifu wa kibiashara wa Umoja huo katika kukabiliana na vita vya kibiashara vya Marekani na katika kukabiliana na hali ya sasa ya "changamoto" ya kimataifa, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Mercosur walipanua kwa muda kutoka 100 hadi 150 idadi ya bidhaa ambazo kila nchi katika kambi hii ya kiuchumi na kibiashara inaweza kusamehewa ushuru wa pamoja wa nje unaotumika na umoja huu wa forodha.

Kukabiliana mataifa ya Amerika Kusini na vita vya ushuru vya Trump

Hatua hii itaruhusu kambi ya kikanda kufanya mazungumzo kwa uhuru zaidi na Marekani na kupunguza athari za ushuru wa 10% wa Trump kwa nchi za Amerika Kusini. Mercosur ina mfumo wa ushuru wa pamoja kwa uagizaji kutoka nchi zilizo nje ya umoja wa forodha, ambayo inakuza mtazamo wa umoja wa kuondoa vikwazo vya biashara ya nje; Ushuru wa Kawaida wa Nje ni ushuru unaolipwa na nchi zinazotaka kuingiza bidhaa zao katika nchi za kambi hii. Kiwango hiki kinatofautiana kutoka sifuri hadi asilimia 35, kulingana na bidhaa.

Siku ya Jumatano, Aprili 2, Trump alianzisha vita kamili vya kibiashara kwa kutangaza ushuru mpya kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje na kuingia Marekani, ambayo wengi wanaona kuwa tishio la kuibuka mgogoro wa kiuchumi duniani. Tangazo la Trump la kutoza ushuru mpya Marekani, ambalo linajumuisha takriban nchi zote, limekumbana na hisia hasi duniani kote.

Kumeibuka radiamali kubwa kuuanzia kwa washirika wa Magharibi wa Marekani, kama vile Umoja wa Ulaya na Kanada, hadi kwa wapinzani kama vile Uchina. Jumla ya nchi 180 zitaathiriwa na hatua hii ya Rais wa Marekani. Hata hivyo, Russia imeondolewa kwenye ushuru mpya kutokana na vikwazo vingi vya Marekani.

Pamoja na hayo, baada ya siku chache, athari mbaya za hatua hii zilipokuwa zikidhihirika, Trump alilegeza kamba ya msimamo wake wa awali na Aprili 9, wiki moja baada ya kutangaza vita vya biashara na ushuru dhidi ya nchi duniani kote, alisema kwamba "atasimamisha kwa muda utekelezaji wa ushuru kwa siku 90 na kupunguza ushuru wa maelewano katika kipindi hiki, na hatua hizi zikitekelezwa mara moja kwa asilimia 10."

Kwa hivyo, nchi nyingi za Amerika ya Kusini zitakabiliwa na ushuru wa chini wa 10%, isipokuwa Venezuela (15%) na Nicaragua (18%). Katika eneo la Amerika Kusini, bidhaa pekee ambazo zitasamehewa na kutojumuishwa na balaa hili ushuru ni shaba, dawa, semiconductur, mbao, dhahabu, nishati na baadhi ya madini.

Kukabiliana mataifa ya Amerika Kusini na vita vya ushuru vya Trump

Hatua hiyo ya Trump ilikuwa jibu la mzozo mkubwa uliofuatia kutangazwa kwa ushuru mpya katika masoko ya fedha nchini Marekani na mataifa mengine duniani, na kusababisha hasara ya zaidi ya dola trilioni 9.

Mjibizo hasi kutoka kwa nchi zote ambazo ushuru huo mpya ulitangazwa pia ulichangia Trump kuangalia upya msimamo wake huo. Amerika ya Kusini ni mojawapo ya kanda ambazo zimekabiliwa na kiwango cha chini cha ushuru kilichowekwa na Trump; ikilinganishwa na Umoja wa Ulaya (asilimia 20) au nchi nyingi za Asia (na ushuru wa zaidi ya asilimia 30).

Kanda hii kwa ujumla inaweza kuwa katika nafasi ya juu zaidi ya washindani wake wa moja kwa moja katika kuingia soko la Marekani, kutokana na vikwazo vya chini vya ushuru. Kwa upande mwingine, wachambuzi wengi wanatabiri kudorora kwa ukuaji wa uchumi wa Marekani kama mojawapo ya washirika wakuu wa kibiashara wa Amerika Kusini kutokana na tsunami ya ushuru ya Trump, ambayo itaathiri moja kwa moja uchumi wa eneo hilo.

Hasa kwa vile uchumi wa Amerika Kusini na Amerika Kaskazini unafungamana sana ukuaji wa uchumi wa Marekani kiasi kwamba, uchumi wa Marekani ukipungua au kudorora, Amerika ya Kusini nayo itahisi hivyo na kupata athari zake.

Filihali nchi za Amerika Kusini ambazo ni wanachama wa Mercosur zimeongeza idadi ya bidhaa zisizo na ushuru kwa uagizaji kutoka nchi zilizo nje ya kambi hii ya kikanda ili kukabiliana na ushuru mpya wa Trump.

Hii itasaidia sana kuongeza vyanzo vya bidhaa kutoka nje kwa nchi hizi na wakati huo huo kupunguza utegemezi wao kwa bidhaa za Marekani. Wakati huo huo, nchi hizi zitakuwa na fursa kubwa zaidi za kusafirisha bidhaa kuelekea Marekani kutokana na ushuru wa 10% kwa wengi wao.

Your Comment

You are replying to: .
captcha