Goff ameeleza hayo katika mahojiano na gazeti la Times alipozungumzia mkakati uliotekelezwa na rais wa Marekani wa wakati huo Joe Biden wakati wa hatua za awali za vita vya Ukraine.
Ukraine iilikuwa ikiomba mara kwa mara ipatiwe mitambo ya kisasa zaidi ya silaha za Marekani lakini hapo awali ilizuiliwa au kucheleweshwa na Washington.
Katika mahojiano, mkuu huyo wa zamani wa operesheni za CIA barani Ulaya na Eurasia amesema, Biden alikuwa akisita kutuma zana muhimu za kijeshi na kivita kwa sababu ya hofu kwamba Russia "itaingia kwenye utumiaji wa silaha za nyuklia".
Goff amedai kuwa uamuzi huo wa kusita kuipatia Ukraine silaha muhimu uligeuza mzozo huo kuwa vita vya muda mrefu na haribifu.
"Kama tungewapa Waukraine silaha zinazofaa wakati huo, wangeweza kuwatimua Warusi hadi nje ya nchi,” ameeleza afisa huyo wa zamani wa CIA.
Goff, ambaye ni muungaji mkono mkubwa wa Ukraine amesisitiza kuwa Marekani na nchi za Ulaya ziliipatia serikali ya Kiev silaha, lakini si za kuiwezesha kushinda vita kati yake na Russia, bali za kuifanya nchi hiyo ivuje damu tu.
Serikali ya Joe Biden ilitoa msaada wa zaidi ya dola bilioni 174 kwa Kiev kufuatia kushadidi kwa mzozo wa Ukraine mnamo Februari 2022, uliojumuisha shehena kadhaa za zana za kijeshi.../
342/
Your Comment