KISA KILIANZA PALE TU MARAFIKI WAWILI WALIKUWA WAKITEMBEA JANGWANI, KATIKA MSAFARA WAO, WALIKIJADILIANA NA KUTOKEA MMOJA WAO KUMPIGA MWENZIE KOFI LA SHAVU, RAFIKI ALIUMIA SAAANA KWA KITENDO HICHO CHA RAFIKI YAKE ILA HAKUTAMKA HATA NENO MOJA BALI ALIANDIKA KATIKA MICHANGA YA JANGWA LILE: LEO, RAFIKI YANGU MPENZI KANIPIGA KIBAO.
MARAFIKI HAO WAWILI WALIENDELEA NA MSAFARA WAO HADI KUFIKIA SEHEMU KWA MAPUMZIKO, RAFIKI ALIEPIGWA KIBAO CHA USONI ULINASA NA KUINGIA MGUU WAKE NDANI YA MICHANGA NA PUNDE TU AKAANZA KUGHARIKI TARATIBU ILA RAFIKI YAKE ILIMSHIKA MKONO NA KUMUONKOA NA MAUTI, NA BAADA YA KUONKOKA ALIANDIKA RAFIKI KWENYE JIWE: LEO, RAFIKI YANGU KAOKOWA MAISHA YANGU.
RAFIKI ALOMPIGA RAFIKI YAKE NA KUOKOWA MAISHA YAKE ALIULIZA: KWANINI MARA YA KWANZA NILIKUPIGA KIBAO ULIANDIKA KWENYE MCHANGA NA SASA HIVI NIMEKUOKOWA UMEANDIKA KWENYE JIWE?
ALIJIMU RAFIKI YAKE: ANAPOTUUDHI MTU TUNAANDIKA KWENYE MCHANGA KIASI YA KWAMBA UKIJA UPEPO UTAVUTA NA ATHARI YA MAANDISHI HAITOBAKI, LAKINI ANAPOFANYA MTU WEMA NI KWETU KUANDIKA KAMA TULIVYOANDIKA KWENYE JIWE KIASI YA KWAMBA HAKUNA AINA YA UPEPO WAWEZA KUVUTA MAANDISHI HAYO.
NDUGU MSOMAJI NINI UMEELEWA KATIKA KISA NA HEKAYA HII?!, TAFADHALI TUONDIKIE MTAZAMO WAKO KWA HESHIMA NA TAADHIMA YAKO.
Na Khamis Sadik