17 Aprili 2013 - 19:30
Je! Mwanamke asokuwa Muislamu aruhusiwa kutumia internet vibaya/Je! Faida ya biashara ya internet ni halali

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(AS)-ABNA- Ayatullah Sistani alijibu baadhi ya maswali kunako shughuli ya internet na utumiaji vibaya Wanawake wasokuwa Waislamu internet.

Ayatullah Sistani katika majibu ya maswali kunako shughuli ya internet je! Ni haramu au la, alijibu kama ifuatavyo:

Swali: Je! ufunguaji internet unatatizo kisheria?

Jibu: Hakuna kiziwizi, ila usiwe utumiaji ndio chanzo cha maasi.

Swali: Mimi ni mmiliki wa internet cafe hujitahidi kuzuiya wale wanaotumia vibaya internet hasa kuingia katika Tovuti mbaya zisiziruhusiwa, ila kuna baadhi huingia kwenye Tovuti hizo kisiri siri, Je! Mapatu yangu kisheria ni halali au la? na nina wajibika kufanya nini?

Jibu: Kama wewe wazuiya watu kuingia kwenye Tovuti mbaya hizo wewe huna kosa,  ila jitahidi kwa kadri ya uwezo wako kuzuiya mambo hayo.

Swali: Je! Yaruhusiwa kuongea na Mwanamke asokuwa Muislamu kwa njia ya internet na kutumia vibaya na kuongea maneno ya kuamsha hisia upande wapili kwa sababu yeye si Muislamu?

Jibu: Kitendo hicho ni haramu na hairuhusiwi.

Swali: Urafiki baina ya Mwanaume na Mwamke kwa njia ya maongezi internet yaruhusiwa bila kuongea maneno ambayo yaweza vutii hisia upande wapili?

Jibu: Kwa sababu yahofiwa kuangukia kwenye haramu hairuhusiwi.

Swali: Hukumu ya kuongea na kuandika kwa njia ya internet ni yepi? Na usoma masomo ya Dini internet yaruhusiwa?

Jibu: Jambo lenyewe halina mushkili kama masomo yatakuwa kutoka Chuo cha Dini hakuna tatizo.