Siku ya leo inasadifiana na tarehe ambayo alizaliwa Swahaba na ndugu wa karibu wa mtume Muhammad s.a.w Ali bin Abitwali ambaye alizaliwa tarehe 13 Rajab, mwaka wa 22 kabla ya hijra sawa na tarehe 20 September mwaka 601 na alifariki tarehe 21 Ramaḍān, mwaka wa 40 hijiria sawa na 27January 661.
Jina lake ni Ali ibn Abi Talib ibin Abd al-Muttalib ibn Hashim ibn
Majina yake maarufu ni: Asadullahil ghalib, Abul hasan, Abu turaab, Amirul Mu’uminiina na mengineyo.
Ali bin Abi twalib ndiye mtu pekee aliyebahatika kuzaliwa katika kaaba tukufu katika mji wa Makka, mama yake alikuwa ni Fatma bint Asad.
Ali ni mtoto wa babake mdogo mtume Muhammad s.a.w, alikuwa ni Mwanaume wa kwanza kusilimu,akitanguliwa na Bi Khadija mke wa mtume s.a.w, ambaye ndiye mtu wa kwanza kuubali uislamu.
Ali aliishi na kulelewa na mtume Muhammad s.aw na alisilimu akiwa na miaka minane,baada ya Ali bin Abitwalib, Abubakar bin Kuhafah alisilimu na kisha maswahaba wengine.
Ali ndiye swahaba aliye muoa Fatma bint wa pekee wa mtume Muhammad s.a.w kwa amri ya Mwenyezi Mungu, ambapo Mwenyezi Mungu aliwaruzuku watoto watano,miongoni mwao ni Hassan na Hussein ambao ni maarufu kama viongozi wa vijana wa peponi.
Katika kipindi chote cha uhai wa mtume Muhammad s.a.w, Ali alitambulika kama msaidizi,mshauri na swahaba wa karibu zaidi wa mtume Muhammad s.a.w, pia alikuwa ni mwandishi wa Qur an tukufu.
Ali bin Abi twalib alisifika kwa ukarimu,upole, elimu hekima na busara ya hali ya juu aliyokuwa nayo, kiasi kwamba mtume Muhammad s.a.w alifikia kusema kwamba:(Mimi ni mji wa elimu na Ali ndio mlango wa mji huo basi atakaye taka elimu yangu lazima apitie kwa Ali bin Abitwalib).
Licha ya kusifika kwa elimu na hekima zake za hali ya juu, Ali bin Abi twalib alikuwa ni Shujaa ambaye hakupatikana mfano wake, mpaka akawa anaitwa Asadullahil ghalib (Simba wa Mwenyezi Mungu mwenye Ushujaa). Pia swahaba huyu ndiye aliagizwa na mtume Muhammad s.a.w kwenda kupambana na majini baada ya majini kuonekana wameasi.
Inasadikiwa kwamba katika kila vita alivyoshiriki yeye peke yake, aliua zaidi ya robo ya idadi ya maadui, hata ikafikia kwamba maadui walipokuwa wakipangwa kupambana na Ali a.s walikuwa wanatoa usia, kwani walikuwa wanajua hawata toka wakiwa salama.
Ali bin Abitwalib ndiye swahaba aliyevunja ng’ome madhubuti ya kambi la jeshi la Mayahudi katika vita vya Khaibar.na kuwa shinda kishindo kukubwa mashujaa wa zama hizo kama vile Marhaba na Amru bin Abdiwud ambao walikuwa ni gumzo na na waliogopwa sana, lakini hakuweza kufua dafu kwa Imam Ali bin Abi twalib.
Ali bin Abi twalib anahesabiwa kuwa ndiye kiongozi na khalifa wa kwanza wa waislamu wa dhehebu ya Shia, ambao wanaamini kwamba ukhalifa na uongozi wa umma wa kiislamu ni haki ya familia ya mtume Muhammad s.a.w. Ali bin Abi twalib ni swahaba pekee aliyetangazwa na mtume Muhammad s.a.w kama msaidizi na kiongozi baada anayemsaidia mtume Muhammad s.a.w.
Mukabala na dhehebu la Sunni ambapo Ali anasadikiwa kuwa ni Khalifa wa nne akitanguliwa na Abubakar,Umar na Uthman.
Ni muhimu kuashiria kwamba, kizazi cha mtume Muhammad s.a.w kinatokana na watoto wa Ali bin Abitwalib na Bi Fatmatu Zahraa, ambapo kizazi hicho hufahamika kama Masharifu, Masayyid,Wajukuu wa mtume na Ahlul bayt.
13 Mei 2014 - 07:42
News ID: 608188

Siku ya leo inasadifiana na tarehe ambayo alizaliwa Swahaba na ndugu wa karibu wa mtume Muhammad s.a.w Ali bin Abitwali ambaye alizaliwa tarehe 13 Rajab, mwaka wa 22 kabla ya hijra sawa na tarehe 20 September mwaka 601 na alifariki tarehe 21 Ramaḍān, mwaka wa 40 hijiria sawa na 27January 661.