23 Mei 2014 - 07:27
kisa chenye mafundisho

Matatizo ni kitu cha kawaida katika maisha ya mwanadamu kwamaana hana ukamilifu, hivyo kitu muhimu ni kutafuta njia sahihi ya utatuzi wa tatizokatika maisha yetu ya kila siku. hiyvo tuwepamoja kuona huyu bwana njia gani anatumia katika kutatua tatizo liliopo baina ya ndugu wawili

Kulikuwa na ndugu wawili walikikaa sehemu moja katika shamba la urithi wa marehemu baba yao, waliishi kwa wema bila ya matatizo baina yao kipindi kirefu , lakini siku moja ikatokea hali yakutoelewana  ambayo ikapelekea kutoelewana nakuwa ugomvi mkubwa nakupelekea kugawa leshamba la urithi, ndugu mdogo kati yao baada ya kugawana urithi hule,kwakukata mawasiliano na kaka yake aliamua kuchimba mto baina ya eneo lake na lakaka yake, kaka yake alipoona hali hiyo ghadhabu ikamzidi, akaketi kufikiria nini afanye dhidi ya ndugu yake ndipo akasikia mtu akigonga mlango,  alipofungua akamuona fundi selemala akiuliza kuwa anayo kazi kwani alikuwa akitafuta kazi. Ndipo mwambia nam kunakazi kidogo hapa, akamchukua mpaka katika ule mto akamwambia angalia huu mto ndugu yangu ameutengeneza ilikukata mawasiliano nami, sasa nataka unitengezee ukuta baina yam to huu ili nisiwe namuona tena, akaenda kumuonyesha ghala la mbao atakazo  tumia katika kazi hiyo naye fundi selemala akaanza kazi yake.
Muda mchache Yule kaka mkubwa alipatwa na haja ya baadhi ya mahitaji ndipo akamwabia fundi kuwa mimi nakwenda mjini kama unamahitaji niambie fundi akasema hapana sina mahitaji, naye akaenda mjini aliporudi akaona fundi ametengeneza daraja katika mto hule , ndipo akaanza kumlaumu kwanini ametengeza daraja baada ya ukuta, walipokuwa katika hali hiyo ndipo ndugu yake akaliona daraja  ndipo moyo wake ukasononeka nakusema nimemkosea kaka yangu kuwa mimi nimetengeza mto kwaajili ya kututenganisha  haliyakuwa yeye ametengeza dara ilikutuunganisha ndipo akapita katika daraja lile nakumkumbatia kaka yake kasha kumuomba radhi.
Wakiwa katika hali hiyo fundi alisimama kando akiwaangalia kisha akakusanya vyombo vyake vya kazi nakuweka begani na kuondoka, Yule kaka mkubwa akamfuata nakumuuliza unakwenda wapi, nakuomba leo uwe mgeni wetu mimi na ndugu yangu! ndipo fundi akamwambia niache niende kwani kunadaraja yingi sana zanahitaji kutengenezwa kati ya mama na mtoto, mtu na rafikiye, baina ya mke na mume nk…. pia nawe waweza kusaidia katika kutengeza daraja hizo!
kwahakika kukosana ni kitu cha kawaida katika maisha ama utatuzi wake  ndio jambo muhimu,  kinachopaswa ni kutafuta njia sahihi ya utatuzi na wala sikuzidisha tatizo.