26 Septemba 2014 - 19:34
Madrasa yafungwa kwa kuhofia usalama Kenya

Maafisa wa usalama nchini Kenya wameifunga Madrasa ya Ngulini kwasababu za kiusalama.

Maafisa wa usalama nchini Kenya wameifunga Madrasa ya Ngulini kwasababu za kiusalama.
Madrassa hiyo iliyo mjini Machakos, Mashariki mwa Nairobi, imefungwa baada ya kugundulika kuwa inawafundisha vijana wa kiislamu itikadi kali za kidini.
Baadhi ya wanafunzi wa madrasa hiyo,wanazuiliwa kwa tuhuma za kuwa na mahusiano na wapiganaji wa kiisilamu wa Alshabab wa Somalia ambao wamefanya jinai kadha wa kadhaa nchini Kenya.
ni ukweli usiopingika kwamba kuna baadhi ya madhehebu ya kiislamu, yanatumia jina la uislamu kufanya ukatili na mauaji, jambo ambalo linapingwa vikali na uislamu halisi, kwani uislamu ni dini ya amani.

Tags