Katibu mkuu wa Hizbollah, Sayyid Hasan Nasrullah amesema kuwa, machafuko na vitisho vilivyopo hivi sasa, haviwezi kutuzuia kufanya maombolezo ya Imam Husein a.s
Sayyid Hasan Nasrullah, ameyasema hayo alipokuwa katika majlis ya kuomboleza masaibu ya yaliyomtokea Husein bin Ali bin Abitwalib mjukuu wa mtume Muhammad s.a.w huko Karbalaa mnamo tarehe 10 Octoba, mwaka 680.
Majlisi hii iliyofanyika katika ukumbi wa Sayyid Shuhadaa,kusini mwa mji wa Beirut, na ilihudhuriwa na viongozi kadha wa kadhaa akiwemo Muhammad Fateh-ali barozi wa Iran Lebanon.
Sayyid Hasan Nasrullah aliongeza kusema kuwa, kumekuwa kukisambazwa uvumi na vitisho vya kutoa mashambulizi kwa waombolezaji wa Imam Husein, huu ni uvumi tu wala haututishi, kwani sisi tunatawakali kwa mwenyezi Mungu mtukufu.
Ni muhimu kuashiria kuwa, Mwaka mpya wa kiislamu hupokewa kwa huzuni na majonzi makubwa kwa wapenzi wa mtume Muhammad s.a.w na kizazi chake, kwani tarehe za mwanzo wa mwaka mpya zinasadifiana na masaibu ya Karbalaa ambayo hatima yake ilikuwa ni kuuawa kinyama Husein bin Ali mjukuu wa mtume Muhammad s.a.w ambaye pia ni imamu na kiongozi wa tatu wa dhehubu la Shia.
26 Oktoba 2014 - 06:28
News ID: 646880

Katibu mkuu wa Hizbollah, Sayyid Hasan Nasrullah amesema kuwa, machafuko na vitisho vilivyopo hivi sasa, haviwezi kutuzuia kufanya maombolezo ya Imam Husein a.s