Eneo ilipo nyumba ambayo Mtume Muhammad (s.a.w) alizaliwa lipo hatarini kufutwa na kujengwa kasri la kifalme. Kazi hiyo ni sehemu ya mradi wa mabilioni ya Paundi kwa ajili ya ujenzi wa katika mji mtakatifu wa Makka ambao umepelekea katika kubomolewa kwa majengo mengi ya kihistoria ya kiislamu mpaka sasa.
Mradi huo ambao umeanza miaka kadhaa iliyopita, unadai nia ya kuutanua msikiti wa mkuu wa Makkah ili kuweza kuhudumia mamilioni ya mahujaji wanaokwenda katika mji huo mtukufu kila mwaka.
Makkah ni mji mtukufu kwa waislamu kwa kuwa kwake ni sehemu alipozaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuwapo kwake kwa Kaaba, Msikiti wa Maka umejengwa kuizunguka Kaaba, na waislamu duniani kote hutekeleza ibada ya swala kwa kuelekea ilipo Kaaba.
Wiki iliyopita Dk. Irfan Alawi wa Taasisi ya uatafiti wa kiislamu yenye makao yake nchini Uingereza alilieleza gazeti la Independent la nchini humo kuwa, majengo yaliyojengwa kama kumbukumbu ya safari ya Mtume kwenda Israi na Miiraj yalibomolewa, majengo hayo yaliyodumu kwa takribani miaka 500, yalijengwa wakati wa dola ya Ottoman ya kituruki.
Mahali alipozaliwa Mtume, maarufu pakijulikana kama Baytul Mawlid, panatarajiwa kubomolewa kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Saudi Arabia inaongozwa na Waflme wenye mlengo wa kiwahabi wa msimamo mkali ambao hupiga marufuku mambo mengi katika namna ya kushangaza.
Ubomoaji wa maeneo ya kihistoria ulitetewa hivi karibuni na Mufti mkuu wa Saudia Arabia Sheikh Abdul Aziz Bin Abdullah al- Sheikh ambapo alisema ubomoaji huo ulikuwa ni wa lazima na kwamba wananchi yawapasa waishukuru serikali kwa kuchukua uamuzi huo, kwa kuwa utaongeza uwezo wa msikiti.
Vyumba vya nyumba alimozaliwa Mtume Muhammada, kwa sasa vipo chini na mwaka 1951 ilijengwa maktaba juu yake ili kuihifadhi. Ambapo baadae ikawekwa alama za kuwaonya mahujaji dhidi ya kuswali wakiwa humo. “ Hakuna ushahidi kuwa Mtume alizaliwa katika eneo hili, kwa hiyo imezuiwa kulifanya eneo hili ni la kuswalia, kuombea dua”, linasema sehemu ya tangazo la onyo katika nyumba hiyo.
Dk. Alawi anasema kuwa “sasa Hijja imekwisha shughuli za ujenzi kwa masaa24 zimeanza tenawamekwisha maliza utanuzi wa msikiti kwa upande mmoja. Jumba la kifalme ambalo litakuwa kubwa zaidi mara tano ya lile la sasa litajengwa katika upande wa mlimani na litakuwa liangalia msikiti kwa chini”.
“kua nzia sasa hadi mpaka Mwezi Disemba maktaba na Nyumba aliyozaliwa Mtume itakuwa haipo tena itakuwa imekwisha potea kabisa na hakuna namna nyingine ya kuzuia hilo”, alisema Dk. Alawi.
Taasisi ya masuala ya mashariki ya kati Gulf Institute, iliyo na makazi nchini marekani imesema kuwa zaidi ya asilimia 95 ya majengo ya kale nay a kihistoria kwa uislamu yaliyokuwapo mjini Makka yamebomolewa yakijengwa mahoteli ya kifahari na na majumba ya kupangisha na maduka makubwa.
Katika mwezi Septemba mwaka huu mpango wa ujenzi wa msikiti wa Mtume uliopo mjini Madina ambao ulikuwa unashauri kuondolewa kwa kaburi la Mtume lililopo ndani ya Msikiti huo ambao ulilalmikiwa na watu wengi duniani kote ilibidi uachwe na serikali hiyo kwa kuhofia hali ya sintofahamu.
Mipango ya mradi huo iliyowasilishwa na Dr. Ali Bin Abdul Aziz al-Shabal kutoka chuo kikuu cha Imam Muhammad ibn Saud, ililetwa mbele ya kamati ya usimamizi wa misikiti miwili, ambapo baadae ulichapishwa katika majarida ya kamati hiyo.