23 Novemba 2014 - 08:27
Wanazuoni wakuu wa ulimwenguni wakutana kujadili hatari ya magaidi wanaochafua jina la uislamu

Wanazuoni wakuu kutokamataifa mbali mbali duniani, wamekusanyika katika mji wa mtukufu wa Qum Iran, ili kujadili hatari inayoukabili uislamu kwa sasa.

Wanazuoni wakuu kutokamataifa mbali mbali duniani, wamekusanyika katika mji wa mtukufu wa Qum Iran, ili kujadili hatari inayoukabili uislamu kwa sasa.

Wanazuoni hao ambao wameitikia mwaliko wa mwanazuoni mkubwa kushia Ayatollah Makarim Shiraz, wamekusanyika kujadili ukweli kuhusu matukio yanayijiri katika ulimwengu wa uislamu. Kwani kumezuka makundi ya watu wanaojinadi na kujifanya waislamu, wanatumia jina tukufu la dini ya uislamu. Wanazuoni hawa leo wamekutana kujadili ukweli kuhusu magaidi wanaotumia jina la uislamu, na kuashiria kwamba uislamu hauwatambui wala kuwafahamu magaidi hao, ingawa wanatumia jina na bendera za uislamu.

Inafaa kuashiria kwamba: vyombo vya habari mbalimbali dunia vimekuwa vikielezea uwepo wa raia wa mataifa ya magharibi miongoni mwa magaidi hao, pia jinai na uhalifu unaofanywa na magaidi hao, si katika mafunzo ya uislamu na kwamba uislamu haujafundisha kuuwa, kubaka wala kudhulumu mali za watu.

Magaidi wa Daesh baada ya kusikia kuweko kikao hiki, wametishia kufanya mashambulizi katika kikao hiki kinachofanyika katika mji mtukufu wa Qum Iran.

Tutaendelea kukupa taarifa ya kikao hiki.

Tags