13 Desemba 2014 - 10:35
Waziri wa Ulinzi wa Ujeruman afanya ziara ya Siri Afghanstani + picha

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen amefanya ziara ya kustukiza nchini Afghanistan, siku chache kabla ya kuondoka kwa wanajeshi wa kimataifa nchini humo.

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen amefanya ziara ya kustukiza nchini Afghanistan, siku chache kabla ya kuondoka kwa wanajeshi wa kimataifa nchini humo.

Waziri von der Leyen ameonya juu ya kuondoka kwa ghafla kwa wanajeshi wa kimataifa, akisema ingawa jumuiya ya kimataifa imepata mafanikio makubwa nchini Afghanistan, hali bado si shwari.

Waziri huyo wa ulinzi ambaye amewatembelea wanajeshi wa Ujerumani katika kambi yao iliyoko Mazaar el-Sharif, amesema jeshi la Ujerumani litachukuwa jukumu la kutoa mafunzo na ushauri kwa jeshi la Afghanistan, baada ya kumalizika kwa operesheni ya kimataifa inayoongozwa na jumuiya ya kujihami NATO.

Ikiwa ni sehemu ya ujumbe unaojulikana kama "Resolute Support" wanajeshi 12,000 wa kigeni watapaswa kubakia nchini Afghanistan, wakiwemo Wamarekani 9000 na hadi Wajerumani 850. Tayari bunge la Ujerumani Bundestag limeidhinisha wanajeshi hao kubakia Afghanistan.

Tags