19 Machi 2025 - 16:38
Tangazo la Urusi la kuwa tayari kupatanisha Pakistan na Afghanistan

Wakati mvutano kati ya Pakistan na Afghanistan ukiendelea, Balozi wa Urusi nchini Pakistan alitangaza utayari wa nchi yake kutatua mivutano hii.

Kulingana na Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul Bayt (AS) - ABNA -; Pamoja na mvutano unaoendelea kati ya Kabul na Islamabad na mapigano ya mpaka kati ya jeshi la Pakistan na vikosi vya Taliban vya Afghanistan, Albert Khorov, Balozi wa Urusi nchini Pakistan, alitangaza utayari wa nchi yake kutatua mivutano hii.

Katika mahojiano na Sputnik, Khorov alisema: Kwa kuzingatia tofauti zilizopo kati ya Islamabad na Kabul, Urusi iko tayari kufanya kazi kama mpatanishi ikiwa pande zote mbili zitapenda (na kuridhia). Muundo wa Moscow unaweza kuwa jukwaa linalofaa kwa hili.

Amesisitiza kuwa: Utatuzi wa mgogoro kati ya nchi hizi mbili kimsingi ni haki ya Islamabad na Kabul, lakini hilo pia ni kwa maslahi ya Russia.

Mwanadiplomasia wa Urusi aliendelea kubainisha: Moscow imeunga mkono mara kwa mara uimarishaji wa hali (ya amani) katika eneo hilo na kusisitiza hitaji la kutolewa mara moja kwa fedha zilizohifadhiwa za watu wa Afghanistan.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha