Waasi wa kundi la Taliban wameuwa watu wasiopungua 19 katika mfululizo wa mashambuzi ya bunduki na kujitowa muhanga nchini Afghanistan leo.
Hii inabainisha kubainisha kuzidi kudorora kwa usalama wakati vikosi vinavyoongozwa na jumuiya ya NATO vikihitimisha kazi yake nchini humo.
Mripuko wa kujitoa muhanga umeliharibu basi la jeshi la Afghanistan mjini Kabul na kusababisha vifo vya wanajeshi wasiopungua sita, wakati afisa wa juu wa idara ya mahakama ameuawa mjini humo mapema leo, na wateguaji 12 wa mabomu ya ardhini wakiuawa kwa kupigwa risasi katika mkoa wa kusini wa Helmand.
Kundi la Taliban limedai kuhusika na mashambulizi yote hayo. Vurugu hizi za karibuni zinakuja kuelekea hitimisho rasmi la vita vya NATO dhidi ya Taliban Desemba 31, baada ya mapigano yaliyodumu kwa miaka 13, ambayo yameshindwa kuzuwia uasi wa kundi hilo la kigaidi.