Shirika la habari la serikali ya China Xinhua, limeripoti kuwa serikali ya nchi hiyo imewakamata zaidi ya watu 30,000 wakati wa msako wa miezi miwili dhidi ya picha za uchi na kamari.
Katika kamatakamata ya hivi karibuni, polisi katika mkoa wa kusini wa Guangdong iliwakamata watu 3,014, na kuwaweka zaidi ya 8,000 katika vizuwizi vya uhalifu kufikia Desemba 15, limeripoti shirika hilo likiinuku idara ya usalama wa umma ya mkoa huo.
Katika mji wa Huizhou, polisi ilinasa mtandao wa kamari unaohusisha dhamana za dola za Marekani milioni 4.82 Novemba 24. Uchezaji kamari ni marufuku nchini China tangu mwaka 1949, ingawa kuna bahati nasibu inayoendeshwa na serikali.
China ilianzisha kampeni dhidi ya picha za uchi mwezi April kama sehemu ya kusafisha mtandao wa Intanet, ambayo ilikwenda sawia na upingaji wa uhuru wa kujieleza mtandaoni, uliyo ongezeka tangu rais Xi Jinping alipochukuwa madaraka mwaka uliyopita.
China ni moja kati ya nchi chache dunia zinazojali maadili ya jamii na kuona kuwa ni wajibu wa serikali kuhakikisha jamii inakuwa na maadili sahihi.
Yafaa kuashiria kuwa nchi nyingi dunian zimeathiriwa na uhuru wa kupita kiasi wa mitandao ya Intanet, nijambo lisilopingika kuwa internet ina faida kubwa sana katika mawasiliano na kurahisisha kazi, lakini pia ina madhara makubwa sana ambayo yanapojitokeza huwa ni vigumu kuyatibu, na kwabahati mbaya wengi wanaitumia intanet kwa maatumizi ya porojo,uhuni na mambo yasiyo na faida, uasherati,wizi,udhalilishaji na hata mafunzo ya vitu vibaya ni moja kati ya mambo ambayo vijana wengi wanajifunza kupitia teknolojia ya intanet.