shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: tarehe ishirini na nane mwezi wa Safari mwaka 13 AH ni siku ambayo alifariki mtume Muhammad (s.a.w.w) pia katika tarehe hiyo kwamujibu wa riwaya zingine ni siku aliofariki Imam Hasan Al-Mujtaba (a.s), kwa matukio haya ya majonzi kwa umma wa Kiislamu nitazungumzia kwa uchache kunako dakika za mwisho za maisha ya mtukufu wa Daraja Muhammad (s.a.w.w) katika kitabu cha Furugh Ibadiyah kilichoandikwa na Ayatulla Jafar Subhaniy Burshiy amenakili kuwa: mji wa Madina ulijawa na khofu na huzuni masahaba wa Mutume (s.a.w.w) wakiwa na majonzi huku wakilia kwa huzuni wakiwa wameizunguka nyumba ya bwana Mtume (s.a.w.w).
katika muda ndipo ikatolewa taarifa kutoka ndani ya nyumba ikiashiria hali ya bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) imezidi kuwa mbaya habari ambayo ilisababisha kupotea matarajio ya kuboreka kwa hali yake, pia habari hiyo kuwasababishia masahaba kusema kuwa baada ya masaa kadha mtume wa amani atatutoka.
Baadhi ya masahaba zake walikuwa wakitamani kuwa karibu na kiongozi wao katika nyakati za mwisho wa maisha ya kiongozi huyo mtakatifu, lakini hali mbaya ya bwana mtume haikuruhusu kutekelezeka suala hilo kwakuwa chumba alichokuwa hakikuwa na nafasi hiyo, isipokuwa AhluBayti zake tu na baadhi ya masahaba walikuwa watakatifu.
Mwana pekee wa bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) bibi Fatima Zahra (a.s) alikuwa ameketi pembeni mwa kitanda cha Mtume na machozi yake yakibubujikwa na machozi huku akishuhudia Mtume (s.a.w.w) akitokwa na jasho la mwisho wa uhai wake, ndipo akawa akisoma mashairi ya kumsifu mtume (s.a.w.w) ambayo yalikuwa yamesomwa na mzee Abu Twalib yakiwa na maana hii: kwa nuru na baraka zake mbingu huteremsha mvua, mtakatifu ambaye makimbilio ya mayatima na mlinzi wa wajane.
Katika kipindi hiki Mtume (s.a.w.w) alikuwa akitokwa na machozi huku akimwangalia Binti yake nakusema: shairi hili alilisoma Abu twalibi katika kunisifu mimi, ama mimi nakusomea aya hii (Muhammad si yeyote kwenu isipokuwa ni Mtume, kwa hakika wamepita kabla yake mitume, endapo akafariki au akauwawa ndio mtarudi katika ukafiri wenu wa awali, na yeyote atakayerudi katika ukafiri wake bila shaka hatamdhuru chochote Mwenyezi Mungu).
Mtume (s.a.w.w) alikuwa akimpenda sana Binti yake Fatima (a.s) kiasi ambacho alikuwa kila anapotaka kusafiri mtu wa mwisho kumuaga ni bibi Fatima (a.s) na kila alipokuwa akirudi safarini nyumba ya kwanza kuingia nakusalimia ni ya binti yake mtakatifu, naye alikuwa akimtukuza zaidi kuliko wengine wote, na alikuwa akiwaambia masahaba wake kuwa (Fatima ni pande la nyama yangu, furaha yake ni furaha yangu na huzuni yake ni huzuni yangu).
Katika kipindi chote cha ugonjwa wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) bibi Fatima alikuwa pamoja naye, na Mtume alipokuwa mwisho wa maisha yake akamwashiria binti yake kuwa kuna kitu anataka kumwambia, bibi Fatima akainama nakukaribisha kichwa chake katika sikio la mtume (s.a.w.w) na wakawa wananong`ona, watu waliokuwa katika sehemu hile walikuwa wanashangaa na kuto elewa wanacho kazungumza, hivyo mtume alipomaliza mazungumzo yake bibi fatima alilia sana, lakini mtume akamnong’oneza tena, ndipo sura ya bibi Zahra ikaonyesha kuwa na furaha nakutabasamu.
Kutokea hali hizo mbili tofauti katika kikao kimoja kiliwataajabisha hadhira waliokuwa hapo, hivyo wakajitahidi kutaka kumuuliza nakujua hakika ya suala hilo alilolifanya bwana Mtume na binti yake.
Fatima Zahra (a.s) akasema (mimi siwezi kufichua sirir ya mtume wa mwenyezi mungu) isipokuwa baada ya kufariki mtukufu mtume Muhammad (s.a.w.w) ndipo alielezea uhakika wa tukio lile kwakusema (kwa mara ya kwanza aliniarifu kuhusu kifo chake na kuniambia kuwa hatapata nafuu katika ugonjwa alio nao, hivyo basi ndio maana nikawa na huzuni na kilio, lakini mara ya pili aliniambia kuwa wewe ndiye mtu wa kwanza katika AhliBayt (a.s) wangu kufariki baada yangu, habari hii ilinipa uchangamfu nakufahamu kuwa baada ya muda mchache nitaungana naye).
Katika hali hiyo mtume akafumba macho yake akisema niitieni ndugu yangu na akae pempeni ya kitanda changu (akikusudia Ally bin Abi Twalib) naye akaja nakukaa pembeni mwa kitanda chake, naye akahisi kuwa Mtume anataka kunyanyuka katika kitanda chake, hivyo akamnyanyua kitandani na kumuegamiza katika kifua chake, muda si mrefu kukatangazwa kuwa hali ya bwana Mtume (s.a.w.w) iko katika hali ya mwisho wa maisha yake.
Mmtu mmoja alimuuliza (Ibuni Abbas) kuwa mtume alifariki akiwa mikononi mwa nani akasema Ibuni Abbas alifariki mikononi mwa Ally bin Abi-Talib, akaendelea kumuuliza kuwa bibi Aisha anadai kuwa mtume alifariki kichwa chake kikiwa kifuani kwangu, ibuni Abbas alipinga suala hilo nakusema (Mtume (d.a.w.w) amefariki mikononi mwa Ally bin Abi-Talib (a.s) naye ndiye aliye muosha akiwa na kaka yangu).
Ally bin Abi-Talib (a.s) katika baadhi ya hutuba zake anaashiria suala hili akisema: kwa hakika amefariki mtume wa Mwenyezi Mungu haliyakuwa kichwa chake kikiwa katika kifua changu... nami ndiye nilisimamia kumuosha na malaika ndio waliokuwa wasaidizi wangu.
23 Desemba 2014 - 13:08
News ID: 660248

Bibi Fatma (a.s) anasema: baba yangu kwa mara ya kwanza aliniambia kunako kifo chake na kunipasha kuwa katika ugonjwa huo hata pata nafuu, hivyo nikaanza kulia na kusikitika katika hilo, lakini kwa mara nyengine aliniambia kuwa wewe ni mtu wa kwanza katika Ahli Baiti zangu watakao ni fuata