28 Desemba 2014 - 13:42
NATO kufanya hafla ya kukamilisha kazi zake Afghanistan

Jumuiya ya Kujihami ya NATO inafanya hafla maalum mjini Kabul ili kukamilisha rasmi operesheni zake za kivita nchini Afghanistan, baada ya miaka 13 ya mgogoro ambao umeiacha nchi hiyo katika kitisho cha kukumbwa na ongezeko la machafuko ya uasi.

Jumuiya ya Kujihami ya NATO inafanya hafla maalum mjini Kabul ili kukamilisha rasmi operesheni zake za kivita nchini Afghanistan, baada ya miaka 13 ya mgogoro ambao umeiacha nchi hiyo katika kitisho cha kukumbwa na ongezeko la machafuko ya uasi.

Hafla hiyo imepangwa kisiri kutokana na kitisho cha mashambulizi ya Taliban katika mji huo mkuu, ambao umekumbwa na miripuko ya mabomu ya kujitoa muhanga na mashambulizi ya watu wenye bunduki katika miaka ya karibuni. Mnamo Januari mosi, operesheni ya kivita ya Jeshi la Kimataifa la Usaidizi wa Usalama - ISAF linaloongonzwa na Marekani litakamilisha shughuli zake. Nafasi yake itachukuliwa na kikosi cha NATO cha kutoa "mafunzo na msaada". ISAF imewapoteza wanajeshi wake 3,485nchini Afghanistan tangu mwaka wa 2001. Takribani wanajeshi wa kigeni 12,500 wanaobakia Afghanistan hawatahusika katika mapigano ya moja kwa moja, lakini watasaidia jeshi na polisi ya Afghanistan katika vita dhidi ya Taliban waliotawala nchi hiyo kutoka 1996 hadi 2001.

Marekani na majeshi mengine ya kigeni nchini Afghanistan yameshindwa kufikia malengo yake katika vita hivyo, hapo awali majeshi ya Marekani yalivamia  kwa lengo la kumtafuta Osama Bin Laden na kusambalatisha mtandao wake wa kigaidi. Lakini mpaka sasa ni miaka kumi na mitatu wanajeshi wa Marekani wamepambana bila mafanikio, na siku baada ya siku magaidi wanaongezeka na kuwa kitisho zaidi.

Tags