30 Desemba 2014 - 09:06
Ndege za Marekani zashambulia kusini mwa Somalia

Ndege za kivita za Marekani zimefanya shambulizi kusini mwa Somalia zikimlenga kiongozi mwandamizi wa kundi la Al-Shabaab. Msemaji wa Wizara ya ulinzi ya Marekani

Ndege za kivita za Marekani zimefanya shambulizi kusini mwa Somalia zikimlenga kiongozi mwandamizi wa kundi la Al-Shabaab. Msemaji wa Wizara ya ulinzi ya Marekani, Admirali John Kirby amesema shambulizi hilo limefanyika jana Jumatatu. Amesema shambulizi hilo limefanyika kwenye eneo la Saakow, siku chache baada ya mkuu wa kijasusi wa Al-Shabaab Zakariyah Ismail Ahmed Hersi, kujisalimisha kwa majeshi ya serikali na Umoja wa Afrika. Hata hivyo, Kirby hajamtaja kiongozi waliyekuwa wakimlenga. Amesema kwa wakati huu hawawezi kutathmini kama kuna raia wowote waliojeruhiwa. Kama kiongozi huyo atakuwa ameuawa kwenye shambulio hilo, litakuwa pigo kubwa kwa Al-Shabaab, baada ya kiongozi wake mwingine Ahmed Abdi Godane kuuawa katika shambulizi jingine la anga la Marekani mwezi Septemba.

Wanamgambo wa Al-shabaab wamekuwa walifanya mashambulizi ya kushtukiza nchini Kenya kwa lengo la kuiadabisha nchi hiyo, ili iweze kurudisha majeshi yake yaloyovamia katika nchi hiyo kwa minajili ya kupambana na wanamgambo hao, ambao ni tishio la usalama wa taifa la Kenya.

Tags