11 Januari 2015 - 11:03
Ofisi ya gazeti yashambuliwa baada ya kumdhihaki mtume Muhammad s.a.w Ujerumani

Ofisi ya gazeti la Hamburger Morgenpost, nchini ujerumani imechomwa moto baada ya kuchapisha vikatuni vya mtume Muhammad s.a.w.

Ofisi ya gazeti la Hamburger Morgenpost, nchini ujerumani imechomwa moto baada ya kuchapisha vikatuni vya mtume Muhammad s.a.w.

Gazeti moja la Ujerumani katika mji wa bandari wa Hamburg kaskazini mwa nchi hiyo ambalo lilichapisha upya vibonzo vya Mtume Mohammad s.a.w kutoka kwa jarida la tashtiti la Ufaransa Charlie Hebdo limelengwa katika shambulizi la kuchoma moto ofisi zake mapema leo. Hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo. Kwa mujibu wa msemaji wa polisi, mawe na kifaa kilichokuwa kikiwaka moto vilirushwa ndani ya ofisi za gazeti hilo kupitia dirishani. Gazeti hilo la kila siku la Hamburger Morgenpost, lilichapisha kwenye ukurasa wake wa mwanzo katuni tatu kutoka kwa jarida la Charlie Hebdo baada ya mauwaji yaliyofanywa katika ofisi za gazeti hilo mjini Paris, na kuweka kichwa cha habari "Uhuru huu mkubwa unapaswa kuwezekana!” Polisi imesema shambulizi hilo lilitokea karibu saa saba na dakika ishirini usiku na kuwa watu wawili wamekamatwa huku vyombo vya usalama mjini humo vikianzisha uchunguzi.

 Vyombo vya habari vya Ulaya vimekuwa vikijaribu mara kadha wa kadhaa kufanya juhudi ya kumdhalilisha mtume wa waislamu Muhammad s.a.w ambaye ni mtu azizi na adhimu sana kwa waumini wa dini hiyo. Nchi za Ulaya zimekuwa zikinadi uhuru wa vyombo vya habari na vimekuwa vikiwafanyia dhihaka viongozi wa nchi mbali mbali havikutosheka vikavuka mpaka mpaka kuanza kudhalilisha manabii ambapo baada ya kufika kwa mtume wa uislamu waislamu wamelipinga vikali jambo hilo.

Jarida la tashtiti la Ufaransa Charlie Hebdo lilichora picha za vikatuni vya kumdhalilisha mtume Muhammad s.a.w na kupelekea shambulizi kali katika ofisi hiyo, ambapo kikundi cha kigaidi cha Al-qaeda kimedai kuhusika na shambulizi hilo na kutoa onyo kwamba wasicheze na hadhi ya mtume Muhammad s.a.w kabla ya moto huo kuzima gazeti hili la Ujerumani nalo limechapisha vikatuni hivyo.

Weledi na wachambuzi wa mambo wanavishauri vyombo vya habari visipewe uhuru w kufanya dhihaka kwa watu watukufu kwani jambo hili litapelekea mashambulizi zaidi ambayo yanaua watu wengine wengi wasio na hatia.

Zaidi ya watu milioni moja wakiwa sanjari na viongozi kutoka nchi takriban 40 wanafanya maandamano kupinga shambulizi lililofanywa na waislamu wenye itikadi kali katika ofisi za gazeti la Charlie Hebdo Ufaransa ambalo lilishambuliwa baada ya kuchapisha vikatuni vya kumdhihaki na kudhalilisha mtume wa waislamu Muhammad s.aw ambaye waislamu wanamheshimu kuliko kiumbe yeyote duniani.

 

Tags