Gazeti la kila wiki la vibonzo la Charlie Hebdo la Ufaransa toleo la kesho Jumatano linatarajiwa kuchapisha kibonzo cha Mtume Muhammad katika ukurasa wake wa mbele chini ya kichwa cha habari "Yote yameshasamehewa"
Walioona kibonzo hicho wanasema Mtume Muhammad ataonekana akishikilia bango lililoandikwa "Je suis Charlie" maneno yenye tafsiri "Mimi ni Charlie, yaliyotumika kuonyesha mshikamano, baada ya shambulizi katika ofisi za gazeti hilo Jumatano wiki iliyopita ambapo wafanyakazi kumi na wawili wa gazeti hilo waliuawa.
Nakala milioni tatu za gazeti hilo la kesho tayari zimeshachapishwa tofauti na kawaida ambapo huwa linachapisha nakala sitini elfu kwa wiki.
Hii inahesabika kuwa ni hatua ya gazeti hili na wafaransa kulipa kisasi dhidi ya shambulio la Pariz lililopelekea watu kumi na wawili kuuawa, ofisi ya gazeti hili inahesabiwa kuwa ndio chanzo cha watu hao kuuawa kwani ilichora katuni za mtume Muhammad na sasa wameamua kuchora na kuchapisha katuni hizo kwa nakala millioni tatu ili kumdhalilisha mtume wa waislamu Muhammad s.a.w.
Tangu mashambulizi ya mjini Paris, mjadala juu ya kuuhusisha Uislamu na vurugu umepamba moto nchini Ujerumani. Lakini mjadala huu unapuuza maono ya mafanikio ya uraia wa Uislamu katika taifa hili, anasema Loay Mudhoon.
Ni dhahiri kuwa mashambulizi ya mjini Paris yameibua maswali yanayoeleweka: Je, Uislamu katika msingi wake ni dini isiyo ya kiutu na inayounga mkono ukatili? Je, mandishi makuu ya dini hii ya ulimwengu yanahalalisha mbinu ya matumizi ya nguvu iliyopitiliza kama inavyoonekana kwa makundi ya jihadi? Na muhimu zaidi ni je, sera ya ushirikishwaji wa Waislamu nchini Ujerumani imeshindwa?
Kwa hakika maswali hayo ni ya haki. Lakini yanapuuza kiini cha tatizo, ambacho ni suala la utangamano wa Uislamu na mafanikio ya kisasa na jamii huru ya kidemokrasia. Lazima ifahamike kwamba hakuna kitu kama Uislamu usiyobadilika. Hakuna mahala popote duniani ambako Waislamu wote wanakuwa na mtazamo sawa.
Katika taifa lolote la Kiislamu, kuna Uislamu tofauti unaofuatwa na kutekelezwa. Kwa mfano, kuna tofauti kubwa kati ya Uislamu nchini Saudi Arabia na ule unaotambuliwa na serikali ya Washia waliowengi nchini Iran. Na katika mataifa ya Kiislamu yaliyofanikiwa kiuchumi kama vile Uturuki na Malaysia, kumejengwa aina ya Uislamu wa wastani wa kihafidhina.
Ukweli huu kuhusu Uislamu unabainisha wazi kuwa ni Waislamu wenyewe wanaoamua juu ya kile wanachokitafsiri kuwa ni Uislamu kulingana na wapi na vipi wanaishi. Uislamu wa madhehebu ya Sunni unaofuatwa na walio wengi zaidi, hauna uongozi wa juu na hauna uamuzi wa mwisho kama alivyo papa katika kanisa katoliki. Na hili linatuongoza kwenye swali muhimu la msingi, ambalo tunapaswa kujiuliza kufuatia mashambulizi ya Paris: Ni Uislamu gani hasa tunapaswa kuwa nao barani Ulaya?
Kwa upande mwingine uislamu wa dhehebu la Shia ndio uislamu unaoonekana kuwa na mpangalio mzuri wenye kukubalika kiakili na unauongozi ulio na misingi thabiti.
Kwa upande wa wakristo pia kuna tofauti kati ya madhehebu ya kikristo pia kuna tofauti kubwa kati ya dini ya Ukristo na dini ya Mayahudi ambao hawana imani na Yesu.
Waislamu ni watu wanaomheshimu sana mtume wao na wanapinga aina yeyote ya udhalilishaji wa mtu huyo mtukufu, tofauti na alivyo Yesu kwa wakristo kwani Yesu kwa wakristo anaonekana ni mtu wakawaida ambaye hata akidhalilishwa hakuna anayeonekana kuumia au kukasirishwa au hata kukemea jambo hilo.
Kutokana na mjadala uliojaa jazba na mabishano, tuko katika hatari ya kupoteza dira ya mafanikio muhimu ya miaka ya karibuni. Kwa sababu kupitia kuingizwa kwenye katiba, Mkutano mkuu wa Waislamu wa Ujerumani DIK mwaka 2005, na kuanzisha mchakato wa kutangamanisha Uislamu na sheria yetu ya msingi, kumekuwa na mabadiliko makubwa sana katika uelewa wa serikali ya Ujerumani kuhusu Uislamu.
Licha ya mivutano na malumbano ya hapa na pale, mchakato huu wa mjadala wa wazi baina ya serikali na raia wake Waislamu, umesaidia kubadili sura ya Uislamu nchini. Hata kama makundi yanayotafuta umaarufu yanautusi Uislamu mara kwa mara na kuutumia kujenga hofu miongoni mwa raia, mafanikio ya sera ya ushirikishwaji hayawezi kukanushwa.
Na hivi sasa tumeshapiga hatua muhimu mbele,kuanzisha masomo ya dini ya Kiislamu katika shule za serikali majimboni. Uanzishwaji wa fani ya theolojia ya Uislamu katika vyuo vikuu vya ndani ni jambo la matumaini na litakuwa nyenzo muhimu ya kujenga Uislamu unaowiana na misingi ya demokrasia ya Ulaya nchini Ujerumani na katika mataifa mengine ya Ulaya.
Kwa sababu Uislamu mara zote umekuwa ukijiambatanisha na wakati wake, na theolojia ya uislam ni matokeo ya nguvu ya kisiasa, serikali na jamii hazina budi kuhakikisha kuwa mchakato wa kujenga Uislamu unaowiana na utamaduni wa Ulaya unaharakishwa. Kwamba jambo hili halina mbadala,imdhihirika kufuatia shambulio la kikatili lililofanywa na magaidi nchini Ufaransa.
Kitendo cha kuchora katuni la mtume Muhammad s.a.w ni sawa na kuchokoza mzinga wa nyuki madhara yake yanawakuta hata wale waliokaa pembeni ambao hawakuhisika na kabisa na kuchokoza mzinga huo.
suali la kujiuliza ni je waislamu wanachukulia vipi msimamo wa serikali ya Ufaransa kuunga mkono kuchora katuni za kumdhalilisha mtume wao, je hii ni hatua ya kutafuta amani, au ni hatua ya kuwachokoza waislamu wenye siasa kali?