17 Januari 2015 - 19:36
Rais wa Ufaransa awatetea waliomdhalilisha mtume Muhammad s.a.w

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema leo kuwa waandamanaji wanaopinga jarida la Charlie Hebdo katika nchi nyingine hawaelewi umuhimu inaouzingatia Ufaransa katika uhuru wa kujieleza.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema leo kuwa waandamanaji wanaopinga jarida la Charlie Hebdo katika nchi nyingine hawaelewi umuhimu inaouzingatia Ufaransa katika uhuru wa kujieleza. Alikuwa akizungumza siku moja baada ya jarida la hivi karibuni la Charlie Hebdo lililo na kikaragosi cha mtume Muhammad s.a.w kuchochea maandamano katika nchi nyingi za Kiislamu duniani. Wakati huo huo, nchi nyingi barani Ulaya zimeimarisha usalama wao baada ya mauaji ya watu 17 mjini Paris,Ufaransa.Ubelgiji imewatuma mamia ya wanajeshi kushika doria katika miji kadhaa kuepusha mashambulizi ya kigaidi baada ya maafisa wa usalama hapo jana kutibua njama ya mtandao wa kigaidi uliopanga kuwashambulia askari na mkuu wa kitengo cha kupambana na ugaidi Mark Rowley Uingereza ametangaza wanatafakari kuchukua hatua zaidi kuwalinda askari wake kutokana na walichokishuhudia katika nchi nyingine barani Ulaya za kulengwa kwa maafisa wa usalama.

Weledi wa mambo wamekosoa kitendo cha rais wa Ufaransa kuunga mkono, waliomdhalilisha mtume Muhammad s.a.w na kusema kuwa serikali yake ndio inayotakiwa kulaumiwa kwa hatari yeyote itakayo jitokeza.

Kuuawa kwa watu 17 nchini Ufaransa kumesababisha hofu kubwa kwa wakazi wa Ulaya, ili hali nchi zao ndio zinazowadhamini magaidi walioshambulia katika tukio hilo.

Nchi za Ulaya zimepanga mikakati dhidi ya raia wa nchi zao wanaorudi kutoka Syria ambao waliruhusiwa kwenda kupambana kuwasaidia magaidi, kwani inaona kuwa raia hao kwa sasa watakuwa ni tishio kwa usalama wa Serikali zao.

Maelfu ya wapiganaji walitumwa kutoka nchi za Ulaya ili kwenda kuiangusha serikali ya Bashar asad wa Syria lakini kutokana na ustadi na uwezo wa jeshi hilo likisaidiwa na jeshi la Jamhuri ya kiislamu ya Iran na wapambanaji mahili wa Hizbollah, magaidi wameshindwa kuiangusha serikali ya Syria ambayo walisema wataiangusha katika kipindi kisichopungua miezi sita, lakini kwa sasa imepita miaka mnne na hakuna hata dalili ya matarajio ya kuiangusha serikali hiyo.

Bunge la Marekani limejadili kuiongezea vikwazo vipya serikali ya jamhuri ya kiislamu ya Iran kwa madai kwamba inaunga mkono magaidi, ikimaanisha inaunga mkono serikali ya Syria na Hizbollah. Na kusahau kuwa wao wanaunga mkono makundi ya kigaidi yanayofanya jinai Iraq na Syria ambayo yameshindwa kuingusha serikali ya Bashar asad na kusababisha hasara kubwa kwa wazamini hao.

 

Tags