19 Januari 2015 - 19:44
Majeshi ya Urusi yaingia Ukraine

Jeshi la Ukraine limedai kiasi ya wanajeshi 700 kutoka Urusi wamevuka mpaka hii leo na kuingia mashariki mwa Ukraine ambako kunaendelea mapigano makali kati ya wanajeshi na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.

Jeshi la Ukraine limedai kiasi ya wanajeshi 700 kutoka Urusi wamevuka mpaka hii leo na kuingia mashariki mwa Ukraine ambako kunaendelea mapigano makali kati ya wanajeshi na waasi wanaoungwa mkono na Urusi. Msemaji wa jeshi la Ukraine Andriy Lysenko amesema leo asubuhi makundi mawili ya wanajeshi wa Urusi yaliingia nchini humo. Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Grigory Karasin amesema Ukraine inajaribu kuutatua mzozo wa mashariki kwa kutumia nguvu za kijeshi na hilo ni kosa kubwa ambalo litauathiri vibaya utawala wa Ukraine. Kumeripotiwa mapigano makali katika jimbo la Donetsk na hospitali moja imeshambuliwa kwa makombora na kuwaacha watu sita na majeraha.Umoja wa Ulaya umesema hautaondoa vikwazo dhidi ya Urusi wakati ambapo mzozo bado unaendelea Ukraine.

 

Tags