10 Machi 2015 - 19:21
Merkel ataka mkataba wa biashara na Japan

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametaka mazungumzo kuhusu mkataba wa biashara huru kati ya Umoja wa Ulaya na Japan yakamilike. Kiongozi huyo ameyasema hayo siku ya pili na ya mwisho ya ziara yake nchini Japan.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametaka mazungumzo kuhusu mkataba wa biashara huru kati ya Umoja wa Ulaya na Japan yakamilike. Kiongozi huyo ameyasema hayo siku ya pili na ya mwisho ya ziara yake nchini Japan. Umoja wa Ulaya na Japan zilifanya duru ya tisa ya mazungumzo kuhusu biashara huru mwezi uliopita, huku mkutano mwingine ukipangwa kufanyika mjini Tokyo mwishoni mwa mwezi ujao wa Aprili. Merkel amekitembelea kituo cha kutengeneza magari cha kampuni ya Mitsubishi Fuso katika mji wa Kawasaki, nje ya mki mkuu Tokyo.

Awali kansela huyo ameitaka Japan kuutafutia ufumbuzi mzozo kuhusu mfumo wa nchi hiyo wa utumwa wa ngono wakati wa vita. Kwa mujibu wa takwimu rasmi wanahistoria wanasema hadi wanawake 200,000 wengi kutoka Korea, China, Indonesia, Ufilipino na Taiwan, waliwatumikia wanajeshi wa Japan katika madanguro ya kijeshi, Japan iliwadhalilisha raia wa nchi hizo jambo lililosababisha chuki kubwa dhidi ya Japan, ambapo nchi hizo zinatafuta sababu tu ziweze kulipa kisasi kwa Japan.