Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Baraza la mawaziri nchini Uturuki limetangaza kuongeza muda wa kile ilichokiita kuwa ni hali ya hatari ya kuendelea kukaa kutumia nguvu za kijeshi hadi mwezi Januari mwakani. Bunge, ambalo linadhibitiwa na chama cha AKP cha Rais Rechep Tayyib Erdogan linatazamiwa kuthibitisha uamuzi huo. Hali hiyo ya hatari awali ilitangazwa tarehe 21 Julai, baada ya jaribio la mapinduzi yaliyoshindwa la Julai 15. Rais Erdogan alisema wiki iliyopita kwamba angeliendelea na hali hiyo angalau kwa mwaka mmoja. Wakati huo huo, kaka wa kiongozi wa Kiislamu, Fethullah Gulen, amekamatwa akishitakiwa kwa kuwa "mwanachama na kiongozi wa kundi la kigaidi." Shirika la habari la serikali linasema kaka huyo aliwahi kushiriki kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa mwaka 2014, akimuunga mkono kaka yake. Takribani watu 35,000 wamekamatwa nchini Uturuki kwa kile ambacho Rais Erdogan anakiita "kung'oa saratani kwenye mfumo".
Mwisho wa habari/ 291