
































Wiki hili limekuwa ni wiki Muhimu kwa waislamu wa madhehebu ya Sunni na Shia kwa kusheherekea siku ya kuzaliwa mtume Muhammad s.a.w ambaye ni mtume wa Mungu aliyeleta dini ya uislamu na kufundisha kitabu cha hekima cha Qur an. Lakini waislamu wa dhehebu la Wahabia au waislamu wa siasa kali wamekuwa wakipinga kuadhimisha siku ya kuzaliwa mtume Muhammad s.a.w wakidai kuwa ni makosa kufanya hivyo. Lakini fikra hizo zinapingwa na mashehe wakubwa waliobebea katika elimu za dini ya kiislamu.