21 Februari 2019 - 08:26
Jeshi la Venezuela laendeleza msimamo wa kuilinda nchi

Waziri wa ulinzi wa Venezuela Vladmir Padrino amesisitiza kwamba jeshi nchini humo litaendelea kuimarisha hali ya tahadhari dhidi ya ukiukwaji wowote kwenye mipaka yake na kwamba linaendelea kumtii Maduro ambaye ni ras Halali kikatiba.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Waziri wa ulinzi wa Venezuela Vladmir Padrino amesisitiza kwamba jeshi nchini humo  litaendelea kuimarisha hali ya tahadhari dhidi ya ukiukwaji wowote kwenye mipaka yake na kwamba linaendelea kumtii Maduro ambaye ni ras Halali kikatiba.

Hatua hii inakuja katika wakati ambapo mpinzani wa rais Maduro, Juan Guaido ambaye ni kibaraka wa Marekani akiongeza shinikizo dhidi ya jeshi kuruhusu kuingia kwa misaada ya kibinadamu nchini humo. 

Amenukuliwa na gazeti la kila siku nchini humo la El Nacional akisema, jeshi lina rais mmoja tu, ambaye ni Maduro. Amesema halitaruhusu serikali ya kibaraka ama maagizo kutoka kwa serikali yoyote ya nje.

Ametoa matamshi hayo baada ya rais Donald Trump wa Marekani anayemuunga mkono Guaido kulionya jeshi la Venezuela siku ya Jumatatu kwamba watapoteza kila kitu iwapo wataendelea kumuunga mkono rais halali Maduro, na kuongeza kuwa watapendelea mabadilishano ya amani ya madaraka, lakini mapendekezo mengine yako mezani.

Maduro arudia kusema Venezuela haina mzozo wa kibinaadamu.

Alirudia tena ujumbe wake kwa rais Trump kwamba Venezuela haina mzozo wa kibinaadamu, kufuatia mwito wa rais huyo wa kuruhusiwa kwa misaada kuingia nchini humo, ambayo hata hivyo misaada hiyo ya wasiwasi ilizuiwa na jeshi la Venezuela.

Colombia imesema kwamba zaidi ya tani 200 za msaada wa dawa, chakula na vifaa vya usafi, nyingi miongoni mwake vikiwa vimetolewa na Marekani vimehifadhiwa katika mji wa mpakani wa Cucuta. Kibaraka Guaido aliapa kuingiza misaada kutoka maeneo mbalimbali kwa njia moja ama nyingine, licha ya vikwazo hivyo vya kijeshi. Misaada hiyo ilitarajiwa kuingia kupitia Brazil na kisiwa cha Curacao.

Hata hivyo, kulingana na gazeti la kila siku la El Universal, kamanda wa jeshi Vladimir Msemaji wa ikulu ya Venezuela amesema, taifa hilo linashirikiana na Marekani kuleta misaada nchini humo, lakini ingewaachia Wavenezuela wenyewe kuichukua kutoka mpakani.

Mwisho wa habari / 291

 

 

Tags