9 Machi 2019 - 05:26
Ujerumani: Hizbullah si kundi la kigaidi

"Vikwazo na orodha ya ugadi ni mbinu mpya ya kulishambulia kundi letu na lazima tukabiliane nao kwa kadri ya uwezo” alisema kupitia hotuba ya televisheni, akitoa wito kwa wafuasi wao kuliunga mkono kundi hilo kwa kutoa mchango. Uwezo wa nguvu za kijeshi wa Hezbollah na umiliki wa aina mbalimbali ya makombora unaipa wasiwasi Israel ambayo imedhulumu ardhi za waarabu ikiwemo Lebanon. Israel ambayo ilijigamba kwa nguvu na uwezo wake wakijeshi kwasasa imejikuta ikijijengea kuta na mahandaki ili kujihifadhi na mashambulizi ya kundi dogo tu la wapiganaji wa Hibullah.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Serikali ya Ujerumani imetangaza msimamo wake kuwa Hizbullah  si kundi la kigaidi, kinyume na Marekani, Uingereza na Israel wanaliona kundi hilo kuwa ni lakigaidi.

Naibu Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Niels Annen ameliambia jarida la habari la Der Spiegel kuwa kundi hilo la Waislamu wa madhehebu ya Shia linaloungwa mkono na Iran si la kigaidi,na ni muhimu katika jamii nchini Lebanon

Matamshi hayo yamekuja baada ya Uingereza mwezi uliopita kulipiga marufuku tawi la kisiasa la Hezbollah, ikilutuhumu kundi hilo kwa kuidhoofisha Mashariki ya Kati.

Hii inatokana na kundi hilo kupambana na Israel pia kupambana na makundi ya kigaidi nchini Syria na Iraq ambayo yanaungwa mkono na Marekani, Uingereza na washirika wao kutoka nchi zaidi ya 60 kwa lengo la kuziangusha serikali za Syria na Iraq, ambapo lengo hilo halikufanikiwa kutokana na kundi hilo kushirikiana na Iran na Urusi katika kutokomeza magaidi hao hatari.

Annen amesema hatua ya Uingereza ni uamuzi wake binafsi na hauna athari ya moja kwa moja kwa msimamo wa serikali ya Ujerumani wala Umoja wa Ulaya. Umoja wa Ulaya tayari umeliongeza tawi la kijeshi la Hezbollah kwenye orodha ya makundi ya kigaidi yaliyopigwa marufuku katika mwaka wa 2013. Hezbollah inawakilishwa katika bunge la Lebanon na inashikilia tatu kati ya nyadhifa 30 za uwaziri katika serikali ya Waziri Mkuu Saad al-Hariri inayoungwa mkono na mtaifa ya Magharibi

Tawi la kijeshi la vuguvugu hilo limeimarisha ushawishi wake katika miaka ya karibuni nchini Lebanon na Syria, ambako pamoja na Iran na Urusi linaunga mkono utawala wa Rais wa Syria Bashar al Assad. Nchini Lebabon, kundi la Hizbullah linazingatiwa kuwa na nguvu zaidi kuliko jeshi la Lebanon kwani kundi hilo kiliweza kuishinda kijeshi Israel ambayo kabla ya hapo ilikuwa ikitambulika kama nchi yenye nguvu zaidi mashariki yakati.

Kiongozi wa Hezbollah atoa ombi la mchango

Mapema Ijumaa, Kiongozi wa Hezbollah Sayyed Hassan Nasrallah alisema nchi nyingine huenda zikaufuata mfano wa Uingereza katika wakati ambao Marekani inaimarisha shinikizo la vikwazo dhidi ya kundi hilo.

"Vikwazo na orodha ya ugadi ni mbinu mpya ya kulishambulia kundi letu na lazima tukabiliane nao kwa kadri ya uwezo” alisema kupitia hotuba ya televisheni, akitoa wito kwa wafuasi wao kuliunga mkono kundi hilo kwa kutoa mchango.

Uwezo wa nguvu za kijeshi wa Hezbollah na umiliki wa aina mbalimbali ya makombora unaipa wasiwasi Israel ambayo imedhulumu ardhi za waarabu ikiwemo Lebanon.

Israel ambayo ilijigamba kwa nguvu na uwezo wake wakijeshi kwasasa imejikuta ikijijengea kuta na mahandaki ili kujihifadhi na mashambulizi ya kundi dogo tu la wapiganaji wa Hibullah.

Mwisho wa habari / 291

Tags