Israel
-
Yemen: Ikiwa Marekani itaingia vitani dhidi ya Iran ili kuisaidia Israel, tutashambulia Meli zake katika Bahari Nyekundu
"Yemen haitasalia kuishia kutizama na kutojali uchokozi wowote dhidi ya nchi ya Kiislamu."
-
Umati wa Wananchi wa Malaysia wameandamana kuonyesha sapoti yao kwa Iran mbele ya Ubalozi wa Marekani Mjini Kuala Lumpur
Hivi karibuni Dunia itashuhudia Haki ikiishinda batili na Imani ikishinda ukafiri.
-
Mshauri wa zamani wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani: Msihadaike, hali ya "Israeli" ni mbaya zaidi kuliko watu wanavyodhani
"Israeli" haikuwa tayari na majibu ya Iran.
-
Gazeti la Wall Street Journal: Israel haiwezi kumudu zaidi ya wiki mbili kwenye vita na Iran
Gazeti hili pia limeelezea kwa kina gharama za vita vya Israel, likisema kuwa gharama za kuzuia kila roketi la Iran kwa kutumia mifumo ya ulinzi wa angani ya Israel zitakuwa kati ya Dola laki saba (700,000) hadi Dola Milioni Nne (4).
-
Sheikh al-Azhar, Ahmad al-Tayeb, amelaani vikali mashambulizi ya uchokozi ya Israel dhidi ya Iran
Kimya cha jumuiya ya kimataifa kuhusu uonevu na uchokozi huu na kukosekana kauli za kuuzuwia, kinachukuliwa kuwa ni ushiriki katika jinai hizo, na matokeo yake pekee yatakuwa ni tishio kwa usalama wa dunia nzima. Vita havizai amani."
-
Uungaji mkono wa vijana wa Fatimiyya kwa majeshi ya ulinzi ya Taifa la Iran, katika haramu tukufu ya Mwanamke wa Heshima, Hazrat Fatima Maasumah (sa)
Uungaji mkono Mkubwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unazidi kuonekana kila Kona ya Dunia katika Operesheni yake ya Ahadi ya Kweli 3.
-
Venezuela: Dunia imefurahishwa na pigo Kali la Iran dhidi ya Utawala wa Kizayuni
Waziri Mkuu wa Venezuela l: "Venezuela inasimama bega kwa bega na Iran katika Haki yake ya kujihami na kuilinda amani yake dhidi ya majaribio yoyote ya jinai za kizayuni".
-
Kiongozi cha Ansarullah Yemen:
"Jinai dhidi ya Iran hata bada ya kusisitiza kuwa haina haja ya silaha za Nyuklia ni kwa sababu ya misimamo imara Iran juu ya kadhia ya Palestina"
Wamagharibi hatwaki kuona Iran ikiwa ni nchi huru, na hii ni kutokana na msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuwatetea wananchi wa Palestina na kukataa udhalimu wa uvamizi wa Kizayuni kwa ardhi za Taifa la Palestina.
-
-
Kukimbia kwa Timu ya Serikali ya Utawala Ghasibu wa Kizayuni (Israel) katika Miji tofauti wakiogopa mvua ya Makombora ya Iran
Hivi sasa, kwa ujumla utaratibu wa vikao vya serikali hii ya Kizayuni ni chini ya ardhi.
-
Ofisi ya Umoja wa Mataifa Tehran: Raia wa kawaida hawapaswi kuwa walengwa kamwe | Tunasimama bega kwa bega na Iran
Ujumbe huo unasisitiza kuwa: "Njia pekee ya kutoka katika mzozo huu ni diplomasia. Kupunguza mivutano na kuendeleza mazungumzo kwa mujibu wa sheria za kimataifa na kwa kuzingatia roho ya Katiba ya Umoja wa Mataifa ndiyo njia salama zaidi ya kulinda maisha ya watu na kuhifadhi amani tunayohitaji."
-
Taarifa ya Pamoja ya Nchi 21 za Kiarabu na Kiislamu Kulaani Shambulio la Israel Dhidi ya Iran
Katika taarifa hiyo, nchi hizo zimetilia mkazo umuhimu wa kuondoa silaha za nyuklia na silaha nyingine za maangamizi ya halaiki kutoka katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Onyo la Jeshi la Iran kwa Walowezi wa Israel | Ondokeni katika Maeneo yote ya Israel haraka ili muokoe Nafsi zenu
Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran linajiandaa na shambulizi kubwa ambalo wameliita kuwa litakuwa ni shambulizi la Kutoa adhabu kwa Adui Israel. Kutokana na hilo imewataka Walowezi wa Kizayuni kutoka ndani ya Israel haraka Sana ili waokoe Nafsi zao.
-
Pezeshkian: Jibu la ujasiri la Mwanahabari wa Kike (Simba Jike) wa Iran lilikuwa ishara ya uthabiti wa Taifa Imara la Iran
Pezeshkiani, alipongeza hatua ya mwandishi huyo wa habari wakati wa matangazo ya moja kwa moja akisema: "Maitikio ya kupongezwa ya simba jike huyu wa Iran kwenye kipindi cha moja kwa moja cha televisheni ni ishara ya upinzani (Muqawamah), uthabiti na kutoweza kushindwa kwa taifa lenye ustaarabu wa muda mrefu dhidi ya kelele za utawala usiojulikana asili yake na usio na sura halali."
-
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu ya Ukaribu baina ya Madhehebu za Kiislamu: "Uhalifu wa Israel ni Jeraha kwenye Mwili wa Umma wa Kiislamu"
Hojjatul Islam Wal-Muslimeen Dakta Hamid Shahriari, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu ya Ukaribu baina ya Madhehebu za Kiislamu ameandika katika ujumbe wake kwenye Twitter yake kuwa: "Uhalifu wa Israel sio tu kuishambulia Iran, bali pia ni jeraha kwenye mwili wa Umma wa Kiislamu."
-
Nchi 11 zalaani uvamizi wa Israel dhidi ya Iran katika kikao cha Baraza la Magavana
Katika taarifa ya nchi kumi na moja wanachama wa Bodi ya Magavana, inachukulia kuwa "shambulio lolote la silaha au tishio dhidi ya vituo vya nyuklia vinavyotolewa kwa madhumuni ya amani ni ukiukaji wa kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa, sheria za kimataifa na Mkataba wa Shirika la IAEA."
-
Waisraeli 24 wauawa na 592 kujeruhiwa katika mashambulizi ya makombora ya Iran katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu
Ofisi ya habari ya Israel imeripoti kuwa, tangu kuanza mashambulizi ya makombora mazito ya Jamhuri ya Kiislamu ndani ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu, Wazayuni 24 wameuawa na wengine 592 wamejeruhiwa.
-
Mashambulio ya kinyama ya utawala wa Kizayuni katika baadhi ya Makazi ya raia Jijini Tehran
Katika siku ya tatu ya uvamizi wake dhidi ya nchi yetu, utawala haramu wa Kizayuni ulilenga baadhi ya maeneo ya Tehran katika mfululizo wa mashambulizi makali.
-
Iran inaendelea Kuichakaza Israel kwa Makombora Hatari ya Balistiki
Wazayuni wanahaha na kutangatanga baada ya Iran kutuma shambulizi la wimbi jipya la Makombora ya Balistiki.
-
Wimbi la Makombora ya Iran Limelenga Ngome za Israel
Mashambulizi haya ya makombora ya balestiki yamesababisha hali ya taharuki kubwa, huku ving’ora vya hatari vikipigwa kote katika maeneo ya utawala huo ghasibu.
-
Kuangushwa kwa Ndege 10 za Kivita za Utawala wa Kizayuni katika Maeneo Tofauti ya Iran
Kamanda wa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatam al-Anbiya(s), ametoa taarifa ya kuangushwa kwa ndege nyingi za kivita za utawala wa Kizayuni.
-
Mashambulizi makubwa ya makombora ya Iran dhidi ya Israel, watu 204 wameuawa na kujeruhiwa, uharibifu mkubwa usiokuwa na kifani katika Mji wa Tel Aviv
Iran, kuanzia usiku wa jana hadi sasa, imevurumisha takriban makombora ya masafa marefu 200 kuelekea malengo mbalimbali katika maeneo ya kati na kaskazini mwa Israel.
-
Tamko la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) kuhusu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) imesisitiza katika tamko lake kwamba: kuanzisha vita dhidi ya Iran ya Kiislamu ni sawa na kuvamia harem (makao matakatifu) ya Ahlul-Bayt (a.s). Katika hali hii, wanaharakati wote wa haki duniani, hasa mashirika na jumuiya zilizo chini ya mwavuli wa Ahlul-Bayt na wale wanaohusishwa na Jumuiya hii, wanaweza sasa kwa sauti kubwa kuliko wakati wowote kusema wazi kuwa utawala wa Kizayuni ni wa kigaidi na mvamizi. Aidha, taifa la Iran, likiwa limeungana zaidi na thabiti kuliko wakati wowote, litatoa jibu kali na la wazi kwa utawala huu wa kihalifu na muuaji wa watoto.
-
Brigedia Jenerali Sayyid Majid Mousavi Ateuliwa Kuongoza Kikosi cha Anga cha IRGC
Katika amri rasmi ya uteuzi, Ayatullah Khamenei amesisitiza umuhimu wa: Kuimarisha uwezo wa makombora na ndege zisizo na rubani
-
Maneno ya Ayatullah Ustadh Abdullah Jawadi Amuli: “Rudisha jiwe, kokote kule lilipotoka"
Ujumbe wa muhimu wa Ayatollah Jawad Amuli kuhusu Jinai ya Kizayuni dhidi ya Iran umetolewa hivi punde.
-
Idadi ya waliouawa Gaza imefikia watu 54,880 | Hali ni mbaya sana na watu wengi wanahitaji msaada wa kibinadamu
Hali ya Gaza inaendelea kuwa mbaya kutokana na mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni. Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa ndani ya saa 24 zilizopita watu 108 wamepoteza maisha na wengine 393 wamejeruhiwa. Jumla ya waliofariki tangu kuanza kwa mashambulizi haya imezidi kufikia watu 54,000. Hali hii inahitaji mshikamano wa kimataifa ili kusitisha ukatili huu na kuanzisha mazungumzo ya amani.
-
Mwakilishi wa Palestina katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa: "Fanikisha kuwasukuma Waisraeli kusitisha mauaji ya kimbari yanayoendelea"
Mwakilishi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amemshitaki utawala wa Kizayuni wa Israel kwa ukiukaji wa sheria za kimataifa na hukumu za Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICC), na kuhimiza hatua madhubuti kutoka kwa nchi za dunia ili kuzuia uhalifu unaoendelea wa utawala huo katika Ukanda wa Gaza. Ametoa msisitizo kuwa mashambulizi yanayofanywa mara kwa mara na Israel dhidi ya raia wasio na hatia na kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia, ni hali inayotakiwa kupokelewa kwa uzito mkubwa na jamii ya kimataifa.
-
Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Mahujaji: "Ulimwengu wa Kiislamu wahitaji kutekeleza mafundisho ya Hija ili kusitisha maafa ya Gaza"
Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa Ulimwengu wa Kiislamu kwa sasa unayahitaji zaidi kuliko wakati mwingine wowote mafundisho ya Hija, na akibainisha kuwa Hija ya mwaka huu ni msimu wa pili unaofanyika sambamba na jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza, ameuliza swali lifuatalo:“Ni nani anapaswa kusimama dhidi ya janga hili la kibinadamu?” Kisha ameongeza kwa kusisitiza: “Bila shaka yoyote, serikali za Kiislamu ndizo zinazobeba wajibu wa kwanza wa jukumu hili, na mataifa ya Kiislamu yana haki ya kudai utekelezaji wa wajibu huo kutoka kwa serikali zao.”
-
Waathirika wa mlipuko wa vipiga simu vya pager nchini Lebanon Washiriki katika uchaguzi nchini Lebanon
Waathirika wa mlipuko wa vipiga simu vya pager nchini Lebanon walishiriki katika awamu ya nne ya uchaguzi wa madiwani wa manispaa (na mitaa) katika maeneo ya kusini mwa Lebanon na kuweka kura zao kwenye sanduku la kupigia kura. Hii ni hatua muhimu ya kushiriki kidemokrasia kwa waathirika hawa ambao wanatumia sauti yao kuleta mabadiliko katika jamii zao.
-
Mazungumzo ya Biashara Huria kati ya Uingereza na Israeli yameghairiwa (yamesitishwa); Balozi wa Israeli London aitwa
Serikali ya Uingereza imeamua kusitisha mazungumzo ya mkataba wa biashara huria na utawala wa Kizayuni kutokana na kuongezeka kwa ghasia zinazofanywa na wakazi wa maeneo ya mizozo na uendeshaji wa operesheni za kijeshi katika ukanda wa Ghaza. Aidha, imeweka vikwazo dhidi ya watu na mashirika yanayohusiana na ghasia hizi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza pia amemwita balozi wa utawala huo ili kutoa maelezo kuhusu hali hiyo na kusisitiza umuhimu wa kuacha mara moja matendo ya ukatili.