-
Umuhimu wa Tabligh, Malengo na Mipango ya Jamiatul - Mustafa (S) nchini Tanzania
Jamiatul - Mustafa ipo tayari kusaidia na kushirikiana na wanaofanya kazi ya kufikisha Ujumbe, Elimu na Maarifa ya Ahlul_Bayt (a.s).
-
Tangazo la Sala ya Eid:
Eid Al_Fitri yatangazwa Tanzania kabla ya kuonekana kwa Mwezi
Mtume (s.a.w.w) ametuelekeza akisema: "Fungeni kwa kuonekana (kwa kuuona) Mwezi, na Fungueni kwa Kuonekana Mwezi". Hivyo tunatarajia kuonekana kwa Mwezi itakuwa ni tarehe 30 au 31".
-
Habari Pichani | Waumini wajitokeze kwa wingi katika Mazishi na Maziko ya Marhuma Ukhti Fatima Mwiru
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-: Hojjat Al-Islam wal Muslimin, Sheikh Dr.Ali Taqavi, na Waumini mbalimbali katika Jiji la Dar-es-salaam - Tanzania, wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika Mazishi na Maziko ya Marhuma Ukhti Fatima Mwiru yaliyofanyika Leo hii Jumamosi (29 Machi, 2025), Maeneo ya Kisarawe - Kimani, Dar-es-salaam - Tanzania.
-
Habari Pichani I Maandamano ya Amani ya "Quds Day" - Dar-es-salaam, Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-: Matembezi ya Quds Day - Ijumaa ya Mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan - Dar-es-salaam, Tanzania.
-
Siku ya Quds Duniani:
Mojawapo ya sehemu ya malengo ya Siku ya Quds Duniani, ni kuienzi Amani ya Dunia nzima
Mojawapo ya sehemu ya malengo ya Siku ya Quds Duniani, ni kuienzi na kuidumisha Amani ya Dunia nzima. Waislamu waishi kwa Amani, Wakristo waishi kwa Amani, na hata Mayahudi waishi kwa Amani, na mtu yeyote asionewe na kudhulumiwa popote pale alipo Duniani.
-
Video | Ripoti ya Mwandishi wa Habari "ABNA" Kwa Lugha ya Kiingereza kutoka katika Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, Katika Mji wa Qom
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - Abna -; Matembezi ya Siku ya Kimataifa ya Quds yalifanyika kwa kuhudhuriwa na matabaka tofauti ya watu wa Mji wa Qom kutoka Madhabahu (Haram) ya Hazrat Maasoumah (s.a) hadi Msikiti wa Quds wa Mji huu. Katika ripoti ya Kiingereza, ripota wa Shirika la Habari la ABNA alishughulikia sehemu ya maandamano haya makubwa kwa kuhoji kundi la washiriki kuhusu motisha yao ya kushiriki katika maandamano hayo.
-
Habari Pichani | Waislamu nchini Burundi wahusha Siku ya Kimataifa ya "Quds"
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA -: Waislamu nchini Burudni, wamejitokeza leo hii katika Siku ya Kimataifa ya Quds na kufanya matembezi ya amani kwa ajili ya kuungana na Dunia nzima katika kuitetea Haki yA Wapalestina na kupinga jinai na udhalimu wa utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi Taifa la Palestina.
-
Video | Imam Baqir (a.s): Amali inayopendwa sana na Mwenyezi Mungu ni ile yenye kudumu hata kama ni kidogo
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA -: Video ikimuonyesha Marhuma Ukhti Fatima Mwiru na sehemu ya Harakati zake za Kiislamu na Kijamii alizokuwa akizifanya na kuzipenda na kudumu katika kuzifanya hadi mwisho wa Uhai wake. Alipenda Wilayat ya Ahlul-Bayt (a.s) na alishikamana nayo daima dawamu, alishikamana na Wilayatul-Faqih, na alifuata na kutetea daima Madhehebu ya Haki ya Ablu-Bayt Rasulillah (s.a.w.w). Allah amfufue pamoja na Muhammad na Aali zake Muhammad (s.a.w.w).
-
Hbari Pichani | Ushiriki Maridhawa Katika Siku ya Kimataifa ya Quds (2025), Khatamul _ Anbiyaa, Arusha, Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA -; Ushiriki maridhawa katika Siku ya Kimataifa ya Quds (2025), umejiri katika Shule za Khatamul _ Anbiyaa, Jiji Arusha, Tanzania, ikiwa ni sehemu ya kuungana na Wanawake, Watoto na wadhulumiwa wote wa Palestina.
-
Habari Pichani | Iran Cultural Center: Semina ya Quds kwa ajili ya Palestina, Jijini Dar _es_ Salaam, Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA -; Taasisi ya Furqan Foundation waandaa Semina ya Quds kwa ajili ya Palestina Jijini Dar _es_ Salaam,Tanzania, chini ya sapoti ya Kitengo cha Utamaduni wa Kiislamu cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dar-es-salaam, Tanzania.