Main Title

source : parstoday
Jumamosi

19 Juni 2021

11:37:13
1151838

Mamilioni ya Wairani washiriki katika uchaguzi wa Rais na Mabaraza ya Miji na Vijiji

Mamilioni ya Wairani wakiongozwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei tangu mapema leo wameelekea kwenye masanduku ya kupigia kura kuchagua Rais wa 13 wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wawakilishi wao katika Mabaraza ya Miji na Vijiji.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alikuwa wa kwanza kutumbukiza kura yake kwenye sanduku la kupigia kura mapema leo katika kituo cha Husainiya ya Imam Khomeini mjini Tehran.

Baada ya kupiga kura Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, siku ya uchaguzi ni siku ya taifa na kuongeza kuwa: Leo wananchi ndio wenye uwanja na medani na kwa kura zao wanaainisha ramani ya nchi kwa ajili ya miaka kadhaa ijayo, hivyo leo ni siiku yao.

Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa, akili na mantiki vinahukumu kwamba wananchi wote wanapaswa kushiriki katika mtihani huu mkubwa wa kitaifa na kwamba zoezi hili la kuchagua rais linawafaidisha wananchi wenyewe na kuipaisha juu Jamhuri ya Kiislamu katika medani za kimataifa. Amesema kura ya kira raia ina umuhimu mkubwa.

Zaidi ya Wairani milioni 59 elfu 310, (milioni 29, 980,000,38 wanaume na milioni 29,330,000, 269 wanawake) wamekamilisha masharti ya kupiga kura katika uchaguzi wa leo wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

342/