Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

4 Aprili 2024

14:18:56
1449045

Raisi: Siku ya Kimataifa ya Quds ni nembo ya kuwatimua Wazayuni katika ardhi za Palestina

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameitaja Siku ya Kimataifa ya Quds kuwa ni ukumbusho wa kukaribia ushindi wa mwisho wa wananchi wa Palestina dhidi ya wavamizi wa Kizayuni na ishara ya mshikamano, umoja na uelewa wa Umma wa Kiislamu katika kutatua kadhia ya Palestina na kuwafukuza wavamizi kutoka katika ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Seyed Ebrahim Raisi ameyasema hayo Jumatano katika kongamano la "Jukwaa la Quds " lililofanyika kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Quds ambalo lilifanyika kwa njia ya video na kuwaleta pamoja  viongozi na shakhsia wa mhimili wa muqawama.

Rais wa Iran amesema: "Busara ya kihistoria ya Imam Khomeini (RA), mwanzilishi mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuitaja Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ni hatua ya kutia moyo na yenye kuunganisha katika kuilinda na kuweka hai kadhia ya taifa la Palestina, kuimarisha mrengo wa muqawama na umoja wa Umma wa Kiislamu.

Raisi ameongeza kuwa: "Maadamu uvamizi wa Quds Sharif unaendelea, kama alivyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu: "Kila siku ya mwaka ni Siku ya Quds."

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kumepatikana matunda katika damu ya mashahidi wa muqawama na pia katika muqawama wa wananchi wa Palestina Gaza. Amebaini kuwa kutokana na bidii, imani na ujasiri wa Wapalestina katika Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, leo imekuwa wazi kwa kila mtu kwamba jumba bandia la Uzayuni ni dhaifu kuliko nyumba ya buibui na ulimwengu unashuhudia kutimia kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu.

Raisi ameeleza kuwa, matukio ya hivi karibuni ya Gaza yameonyesha kuliko wakati mwingine wowote kwamba utawala ghasibu wa Kizayuni haufuati kanuni zozote za kibinadamu, kimaadili, kisheria na kimataifa na huchukua hatua za kinyama na zisizo za kibinadamu ili kuficha udhaifu wake wa ndani.

342/