8 Juni 2024 - 18:25
Sisitizo jingine la Iran na Azerbaijan la kutekeleza makubaliano ya nchi mbili

Katika mazungumzo yake ya simu na Kaimu Rais wa Iran, Mohammad Mokhber, sambamba na kutoa salamu za rambirambi kwa taifa la Iran kutokana na kuondokewa na Rais Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Azerbaijan, Ilham Aliyev, ameeleza mshikamano wake na serikali na wananchi wa Iran.

Rais wa Azerbaijan amekitaja kifo cha Seyed Ebrahim Raisi kuwa ni kikubwa na hasara kwa nchi na mataifa yote ya Kiislamu katika eneo hili.

Rais wa Jamhuri ya Azerbaijan pia ameashiria mashauriano na makubaliano yake na Shahidi Seyed Ebrahim Raisi katika kikao cha mwisho baina yao, na kueleza kwamba, utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano huo yatapelekea kukuza uhusiano na ushirikiano wa pande zote. Kadhalika amesema, miongoni mwa makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa katika mkutano na shahidi Raisi ni kufunguliwa ubalozi wa Azerbaijan mjini Tehran, ambao utafanyika hivi karibuni. Ilham Aliyev pia alisisitiza kuwa atajitolea kwa ajili ya ushirikiano wa kikanda na kuepusha uwepo wa wageni katika eneo hili.

Baada ya tangazo la uhuru wa Jamhuri ya Azerbaijan mnamo Oktoba 1991, Iran ilikuwa moja ya nchi za kwanza kutambua uhuru wa nchi hiyo. Baadaye, viongozi wa Tehran na Baku walitiliana saini mamia ya hati za makubaliano katika miongo mitatu iliyopita. Mikataba hii ambayo ilitiwa saini hasa kutokana na msisitizo wa viongozi wa serikali ya Baku katika masuala ya usalama, kutoingilia masuala ya ndani ya kila mmoja wao, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, kuingia na kutoka kwa urahisi raia wa nchi hizo mbili na masuala mbalimbali ya mipaka ambayo mingi yake bado haijatekelezwa.

Vyovyote itakavyokuwa, mipango mipya ya Iran na Jamhuri ya Azerbaijan katika uga wa ujenzi wa mabwawa na ujenzi wa barabara na njia za reli ni mipango muhimu na ya kistratejia ambayo utekelezaji wake utapelekea ustawi wa kiuchumi wa nchi hizi mbili jirani za Kiislamu.Hatupaswi kuacha kusema hapa kwamba, mwenendo wa matukio katika Caucasus Kusini na utatuzi wa migogoro kati ya Armenia na Jamhuri ya Azabajani imeambatana na matatizo mengi hadi sasa. Kutatua mizozo hii kutakuwa na athari kubwa kwa ushirikiano wa serikali na mataifa katika kanda. Katika hali ya sasa, pande hasimu zinajaribu kujadiliana na kushauriana ili kufikia amani na utulivu wa kudumu katika eneo hilo kwa kuainisha mipaka na kupiga hatua moja mbele kuelekea amani ya kudumu na hivyo  kurejesha amani na utahabiti katika eneo.

Hii ni katika hali ambayo, sehemu kubwa ya mpaka kati ya Iran na Jamhuri ya Azabajan inaundwa na mto wa mpakani wa Aras kama mpaka wa asili. Ni dhahiri kwamba wakati wa kukaliwa kwa mabavu Karabakh na miji 8 ya Jamhuri ya Azabajan, karibu kilomita 80 za mpaka wa pamoja wa nchi hizo mbili kando ya Mto Aras zilizingatiwa kuwa ardhi zilizoteketezwa.

Kuhusiana na hili, "Bahram Amir Ahmadian", profesa wa chuo kikuu na mtaalamu wa masuala ya Caucasus, anasema: "Kuanza operesheni ya kijeshi ya Jamhuri ya Azabajani kwa ajili ya kurejesha maeneo yaliyochukuliwa ya Karabakh mnamo Novemba 2020, kulipelekkea eneo la Caucasus Kusini likabiliwe na mabadiliko makubwa." Kwa mujibu wa mtaalamu huyu wa Iran ni kwamba, "wahusika wa kikanda na wa nje wameshiriki katika matukio hayo, ambayo yalisababisha kuvurugika kwa uwiano wa kieneo, hususan kwa Jamhuri ya Kiislamu, jambo ambalo limekuwa na taathira hasi kubwa katika uhusiano kati ya Iran na Jamhuri ya Azerbaijan. ".

Hii ni pamoja na ukweli kwamba, wakati wa vita na baada yake, tofauti na mizozo ya hapo awali, vikosi vya jeshi la Iran vimesimamia kwa uangalifu na umakini mipaka ya pamoja na nchi hasimu na jirani.

Kiujumla inapasaa kusema: Matamshi ya Rais wa Jamhuri ya Azerbaijan katika mazungumzo ya simu na Kaimu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu yanapaswa kuzingatiwa kama hatua nyingine ya viongozi wa Baku kwa ajili ya kubadilisha mchakato wa ushirikiano na nchi jirani na ya Kiislamu, ambayo daima imekuwa ikikimbilia kusaidia nchi hii ya Kiislamu yaani Jamhuri ya Azerbaijan.

Inatarajiwa kwamba kwa kutekelezwa miradi ya barabara na reli na kuzinduliwa kwa ukanda wa kimkakati wa Kaskazini-Kusini, nchi kama Jamhuri ya Azabajani, zitafungua njia nyingine muhimu ili kushirikiana na sehemu muhimu ya dunia yaani, bara kubwa la Asia.



342/