Rais Pezeshkian amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambaye aliiomba Iran kujizuia katika tukio la kuuawa Ismail Haniyeh aliyekuwa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na kuongeza kuwa, Iran daima imekuwa na nafasi muhimu katika kuleta amani, utulivu na usalama katika eneo na dunia na kuzuia mivutano, ukosefu wa usalama na vita.
Pezeshkian ameeleza kuwa, Utawala wa Kizayuni unajaribu kuwasha moto katika eneo kwa vitendo vyake vya kigaidi dhidi ya watu wasio na ulinzi wa Gaza, na kwa bahati mbaya, Marekani na nchi za Magharibi zinauunga mkono utawala huo katika kutekeleza jinai, mauaji ya kimbari na ugaidi badala ya kulaani.Rais wa Iran amesema: Maadamu utawala wa Kizayuni unafanya mauaji ya kimbari, jinai na ugaidi kwa uungaji mkono wa kisiasa, kifedha, silaha na vyombo vya habari vya Marekani na nchi za Magharibi, eneo na ulimwengu hautashuhudia utulivu, usalama na amani.
Rais wa Iran amesema bayana kwamba, kama Marekani na nchi za Magharibi zinataka kweli kuzuia vita na ukosefu wa usalama katika eneo hili, ili kuthibitisha madai hayo, basi zinapaswa kuacha mara moja kuuzia silaha na kuunga mkono utawala wa Kizayuni na kuulazimisha utawala huo kusimamisha mauaji na mashambulizi ya kimbari dhidi ya Gaza na kukubali kusitisha mapigano.
342/