Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

8 Agosti 2024

15:10:25
1477384

Iran yalaani nchi za Magharibi kukosa uungwana mbele ya jinai za Israel

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezilaumu nchi za Magharibi na kusema kuwa zimepoteza heshima na itibari yao mbele ya vita vya Ghaza na zimeshindwa kuonesha hata uungwana wa kiwango cha chini kabisa katika vita hivyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, Nasser Kan'ani amesema hayo katika mtandao wa kijamii wa X na kuongeza kuwa, katika kamusi ya Marekani na Ulaya, wananchi na makundi ambayo yanapigania ukombozi wa ardhi zao mbele ya uvamizi wa maajinabi; watu na makundi ambayo yanapigania usalama wa nyumba zao, familia zao na heshimao zao mbele ya jeshi katili na vamizi ambalo limejiandaa kwa silaha zote kali, watu hawa katika kamusi ya Marekani na Ulaya ni magaidi na kwamba upande wowote unaosimama pamoja na watu hao eti nao unaunga mkono ugaidi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa, katika kamusi hiyo ya Marekani na Ulaya, dola pandikizi, ambalo hadi hivi sasa limeshaua kidhulma zaidi ya raia 40,000 katika kipindi cha miezi 10 tu huku karibu 10,000 kati yao wakiwa ni watoto wadogo, dola hilo kwa mtazamo wa mabeberu hao si la kigaidi, bali linapaswa kupongezwa na kila mtu, na kupewa uungaji mkono wote wa kisiasa, kiusalama, kijeshi na kisilaha. Magharibi imepoteza itibari na heshima yake katika vita vya Ghaza na imeporomoka vibaya kimaadili.

Zaidi ya siku 300 zimepita tangu utawala katili wa Kizayuni ulipoanzisha mashambulizi ya kikatili ya pande zote dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Ukanda wa Ghaza. Israel isingeliweza kuendelea na jinai hizo kama si kwa uungaji mkono wa kila upande wa madola ya kibeberru ya Magharibi hasa Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani. 

342/