Kulingana na ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul_Bayt (a.s) - ABNA - Satelaiti ya kupima (na kuchunguza) ya "Kowsar" na Satelaiti "Hod-Hod" zilizinduliwa kwa kutumia kirusha Satellite cha "Soyuz" cha Urusi kutoka kituo cha "Vostochny" mapema leo hii Jumanne, Novemba 5, 2024, na zote mbili ziliwekwa kwa mafanikio kwenye Orbiti.
Mkuu wa Shirika la Anga la Iran, baadhi ya Wanachama wa Timu ya utengenezaji wa Satelaiti na Waandishi wa Habari katika Taasisi ya "Utafiti wa Anga ya Juu ya Iran" walitazama matangazo ya moja kwa moja ya uzinduzi huu kwa namna inayotarajiwa na kushuhudia uzinduzi wake ukiwa ni wenye mafanikio makubwa.
Satelaiti ya "Kowsar", ambayo ina uzito wa Kilo 30, na ambayo Umri wake wa (kuishi au kukaa) ndani ya Orbiti inakadiriwa kuwa ni zaidi ya miaka 3.
Ina Camera katika wigo wa "NIR na RGB" na ni Satelaiti ya kwanza ya Iran yenye azimio la wastani la mita 3.45 GSD - Ground Sampling Distance - (Umbali wa Sampuli ya Ardhini ), ambayo ina maana ya Satelaiti yenye maendeleo ya juu zaidi hadi kufikia mwaka 1400 ndani ya Iran.
Satelaiti ya "Kowsar" inafaa kwa matumizi ya kilimo, ramani na uchunguzi (utafiti), na anuwai ya picha za rangi ni kwa umbali wa kilomita 15, na kiwango cha picha ni fremu 6 kwa sekunde moja, na Umri wa Wastani wa timu (ya wataalamu) iliyounda Satelaiti hii ni miaka 26.
Muda cha orbiti wa Satelaiti hii ya Kowsar ni Sekunde 5,677 na uzani wa jukwaa lake unafikia kiwango cha juu cha kilo 35.
Usahihi wa kuashiria (The Pointing Accuracy) wa Satelaiti hii ni sawa na digrii 1 na usahihi wake wa uthabiti ni digrii 0.05 kwa sekunde.
Kowsar ina uwezo wa uzalishaji wa saa 44 watt na uwezo wa matumizi ya saa 29 watt, ambayo hutumiwa kutoa nishati kwa ajili ya usafirishaji.
"Hodhod" ni Satelaiti iliyo na kiwango cha Satelaiti za ujazo, na dhamira (kazi) yake ni kuunda jukwaa maalum la kutoa "Huduma za Kimataifa za Mtandao wa Mambo" /Internet of Things (IoT).
Huduma za Satelaiti za Hud_Hud (au: Hod-Hod) zinazotumiwa sana ni katika nyanja za Kilimo, Usafirishaji, Logistiki na Mazingira.
Uzito wa Satelaiti hii ni Kilo nne (4), na urefu wake wa Orbiti ni Kilomita 500, na Umri wake wa (ndani ya) Orbiti ni miaka minne (4), na inatumiwa kwa madhumuni ya Kilimo na utoaji wa ramani (ya Milima na Misitu).