Main Title

source :
Jumamosi

19 Machi 2011

20:30:00
270794

Itikadi sehemu ya kwanza

Akida

AKIDA Akida ni moja kati ya elimu muhimu kwa kila muislamu, elimu hii inaongelea (mizizi ya dini) au itikadi za kiislamuambazo kila muislamu anatakiwa kuwa na imani nazo. Kwa jina jingine, elimu hii huitwa “Kalaam” (Islamic Theology). Kwa mukhtasari tunaweza sema kuwa: Elimu hii inazungumzia misingi ya dini ya kiislamu (Usuulu din)

  DHIMA KUU YA ELIMU HII:•Kuchambua:Moja ya dhima za mwanakalaam ni kurejea maandiko matukufu Qur an na hadithi) na kuzichambua itikadi za kiislamu). •Kuelezea:Baada ya kuzichambua itikadi hizo mwanakalaam anatakiwa kuzielezea kwa lugha ambayo itafahamiwa na mlengwa. •Kupangilia:Kutokana na kwamba, aya na hadithi zinazoongelea itikadi za kiislamu, zimeshushwa katika sura tofauti, ni wajibu wa mwanakalaam kuzikusanya na kuzipangilia kwa mpangilio wa kimantiki ili kurahisisha ufahamu wake.•Kulinda misingi ya dini ya kiislamu:Hii ni katika dhima nzito na ngumu ambayo mwanakalaamu anatakiwa kuifanya.   Mwanakalaamu anatakiwa awe na uwezo wa kuzitetea itikadi za kiislamu dhidi ya maadui, pia dhidi ya shubuhaati (Maswali ya kutatanisha) kwa kutumia maandiko matukufu na hoja za kimantiki na falsafa.MWANA KALAAM:   Tukitazama kwa makini dhima kuu za elimu hii, bila shaka tutakuwa tumesha mtambua mwanakalaamu ni nani?   Sitapenda kuichambua zaidi mada hiyo kwani itakuwa ni marudio, ila nitataja  baadhi ya elimu ambazo mwanakalaam anapaswa kuzibobea ili aweze kutekeleza wadhifa wake. Miongoni mwa elimu hizo ni:•Qur an.•Hadithi.•Fiqh.•Tarekhe (historia).•Mantiki.•Falsafa.•Lugha ya Qur an na Hadithi, pia lugha ya watu anaotaka kuwafikishia ujumbe. Licha ya elimu hizi mwanakalam anatakiwa kuzifahamu elimu nyingine pia, ambazo kutokana na ufinyu wa mada hii, sitaweza kuzitaja.MAKUNDI NA MADHEHEBU YA KALAAM  Tukiangalia elimu ya fiqh ambayo inaongelea (matawi ya dini) au mambo ambayo muislaamu anayopaswa kuyafanya) tunakuta makundi mengi, nahii inatokana na tofauti za mitazamo ya wanazuoni na maulamaa wa elimu hii. Baadhi ya makundi hayo ni:JAAFARII au Mashia,ZAIDII,HANAFII,SHAAFII,MALIKII,HANBALII.ambapo kila moja katika makundi haya lina mtazamo wake katika maswala ya kifqh.   Kama vile ambavyo elimu ya fiqh inamakundi tofauti, vivyo hivyo Elimu ya kalaamu, na sababu kuu ni ileile, ambayo ni tofauti ya mitazamo ya maulamaa wa wanazuoni wa elimu hii.Makundi na madhehebu muhimu ya wanakalaam ni:MASHIA, MU’UTAZILAH, ASHAAIRAH NA MURJI’E.ATHARI NA MATATIZO YA MAKUNDI HAYO.  Kama tulivyo tanguliza kuelezea hapo juu, kwamba sababu ya makundi haya ni tofauti za mitazamo ya wanazuoni na maulamaa. Kwa muhtasari, nitapenda kuelezea athari za mgawanyiko na makundi haya katika uislamu:•Mgawanyiko na makundi katika elimu ya fiqh; ndio sababu kuu ya matendo ya waislamu kutofautiana, ambapo unakuta kundi moja linasisitiza na kuamrisha kitu Fulani na lingine linapinga au kutoa hiari. Mfano: kuweka mikono kifuani wakati sala, kuna makundi yanasisitiza kuweka mikoni kifuani katika sala na mengine yanaharamisha kabisa kitendo hicho, kundi lingine linasema unahiari unaweza weka mikono kifuani pia unaweza acha kuweka.•Mgawanyiko katika makundi katika elimu ya kalaam; ndio sababu kuu ya itikadi za waislamu kutofautiana, nahii ndio sababu kubwa ya baadhi ya makundi ya kiislamu kukafirisha, ambapo unakutakundi moja linatuhumu kundi lingine ni kuwa ni makafiri kwa kuwatu limekwenda kinyume na mtazamo wake. Sitapenda kuzungumzia kwa undani zaidi mambo haya, kwani hapa si mahala pake.Katika mada zijazo insha’allah nitajaribu kuelezea na kuchambua makundi ya kalaam na itikadi zao kwa muhtasari.