Main Title

source :
Ijumaa

20 Juni 2014

16:57:04
617589

sehemu ya tatu

Ukweli kuhusu Kifo

Je, Uhalisia wa mwanadamu ni mwili wake? Kiasi kwamba sehemu ya mwili ikipungua au kutoweka je? itamaanisha kutoweka,kupungua sehemu ya ubinadamu wake?

 

FAIDA ZA KIFO:

 

  • Kufahamu umuhimu na thamani  Uhai: kifo kimekuwa ni sababu ya watu kujali na kufahamu umuhimu wa maisha na uhai.

 

  • Kufahamu umuhimu wa muda: kifo kimekuwa ni sababu ya watu kufahamu umuhimu wa muda na kutoupeteza bure. Ifahamike kwamba ikiwa mtu amepangiwa kuishi miaka 10, kila sekunde ni hatua kuelekea mwisho wa uhai wake, hivyo mwenye kulitambua hilo hawezi poteza muda kwa kufanya mambo ya upuuzi.

 

  • Sababu ya kupatikana nidham na mpangilio: kifo kimekuwa ni sababu ya kupatikana nidhamu na mpangilio kwani bila kifo mpangilio ungeharibika, kwa mfano mtu angejisikia kumgonga mwingine na gari bila shaka wala wasi, watu wangejiachia kwenye milima, wangefikia hata kuwachezea simba sharubu zao.

 

  • Mabadiliko ya kitabia na uadilifu: Uoga wa kifo ndio sababu ya watu kubadilika kitabia na kuwa na maadili ya kibinadamu. Kifo kimesabisha watu wenye kiburi na fahari kushuka chini na kupunguza kiburi chao, majingambo ya mali na uzuri  mara tu wafikiriapo kuwa baada ya muda watakuwa ni mizoga yenye kutoa harufu na kwamba si mali, nguvu wala umashuhuri wenye kuweza  kuwaokoa na kifo.

 

  • Kupatikana elimu: Fikra ya kifo ndio imekuwa sababu ya kuchimbuka elimu mfano wa Falsafa na hata baadhi ya dini,kwani wanafalsafa walianza na kufikiria sababu ya kifo kisha wakaanza kuchambua kama tumepangiwa kufa kwanini tumepangiwa kuishi?  Majibu ya swali hili yalisababisha kupatikana elimu kadhaa wa kadhaa.

 

Nitapenda kumalizia kwa kauli ya mtume Muhammad s.a.w:  Yatumie vizuri mambo manne kabla ya manne:

 

     1. Ujana kabla ya uzee.

 

    2. Afya kabla ya maradhi.

 

    3. Utajiri kamba ya ufukara.

 

    4. Uhai kabla ya kifo.

 

Hakuna maana kuogopa kifo, badilika kitabia kuwa na maadili sahihi ishi kwa raha ufe kwa raha.