Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA kupitia Russia Al-Yaum, Dmitry Medvedev, Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Urusi, alisisitiza kuwa kutekwa kwa rais wa Venezuela na Marekani hakuna uhusiano wowote na suala la biashara ya dawa za kulevya, bali suala ni mafuta pekee, na maafisa wa Marekani wamekiri hilo waziwazi.
Akijibu matamshi ya Trump kwamba Marekani itachukua utawala wa Venezuela, aliongeza kuwa Marekani haiwezi kuitawala Venezuela kutokea mbali. Medvedev aliongeza kuwa, huenda Marekani ikawa na nia ya kurudia operesheni hii dhidi ya utawala wa Kiev. Alisema hatua za Marekani ni haramu lakini zinaendana na sera za kudumu za Washington za kudhibiti rasilimali za nchi nyingine, jambo ambalo linaonekana pia katika rasilimali adimu za madini za Ukraine.
Your Comment