Shambulio dhidi ya mzee mmoja katika mji wa Torrepacheco katika eneo la Murcia nchini Uhispania limezusha wimbi la ghasia za kibaguzi, huku makundi ya mrengo wa kulia yakitumia tukio hilo kuchochea chuki dhidi ya wahamiaji wa Morocco. Ripoti hii inachunguza chimbuko la tukio, matokeo yake na juhudi zinazoendelea za kudhibiti mgogoro huo.
Sambamba na ufunguzi wa Ofisi ya kikanda ya Shirika la habari la ABNA nchini Ghana, vyombo vya habari vya nchi hiyo vilikaribisha uwepo wa chombo hiki cha habari cha kimataifa na kukitambulisha kama jukwaa la kusambaza simulizi za kitamaduni na kidini kutoka ulimwengu wa Kiislamu hadi Afrika Magharibi.