Zama
-
Mufti wa Misri Atoa Onyo Kuhusu Mkanganyiko wa Taarifa: Ni Muhimu Kuzitafsiri Upya Thamani za Kiislamu kwa Lugha ya Kisasa
Nazir Muhammad Ayyad, Mufti wa Jamhuri ya Misri, akisisitiza umuhimu wa kuzitafsiri na kuziwasilisha upya misingi na thamani za Kiislamu kwa lugha ya zama hizi, pamoja na kuziunganisha na masuala ya vyombo vya habari vya kidijitali, mitandao ya kijamii na akili mnemba (AI), amesema kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuimarisha uelewa wa kijamii na kukabiliana na mkanganyiko wa taarifa unaoikabili dunia ya leo.
-
Wanafiki Walikuwa Wanatambulikaje? Jibu la Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na Maswahaba kwa Swali Moja la Kihistoria
Katika zama ambazo wanafiki walikuwa wakijitahidi kuficha sura zao halisi, ni jambo gani lililokuwa likifichua unafiki wao? Riwaya zilizopokewa kutoka kwa Maswahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) zinaonesha kuwa chuki na uadui dhidi ya Amirul-Muuminina Ali bin Abi Talib (a.s.) vilikuwa miongoni mwa viashiria muhimu vya kuwatambua wanafiki katika zama za mwanzo za Uislamu.
-
Ayatollah Ramezani:
Allamah Sayyid Jaafar Murtadha Amili Alikuwa Mwanazuoni Mashuhuri Zaidi wa Zama za Sasa katika Utafiti Upya wa Kihakiki wa Historia
Ayatollah Ramezani, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (as), katika kikao cha kumuenzi Allamah Sayyid Jaafar Murtadha Amili, amemtaja kuwa miongoni mwa wanazuoni mashuhuri na makini zaidi wa zama za sasa katika kufanya uhakiki na kuijenga upya historia ya Ahlul-Bayt (as). Amesisitiza kuwa mwanazuoni huyo mkubwa, kwa kutumia mbinu ya kielimu inayotegemea ijtihadi, aliisafisha historia ya Uislamu kwa kuondoa simulizi zisizo na ushahidi wa kutegemewa pamoja na visa vya kubuni vilivyoenea katika jamii.
-
Makala ya Tafakuri: Familia ya Fatima (SA); Kuanzia Mbinu za Kuiga Mfano Wake Hadi Nguzo za Maisha ya Kifatimiyya Katika Zama Zetu
“Familia ya Fatima (SA)” si jamii bora ya kufikirika iliyo mbali, isiyoweza kufikiwa au iliyofungwa ndani ya historia ya zamani. Bali ni mfumo hai, wenye nguvu na unaofaa kwa nyakati zote, ambao unaweza kutekelezwa katika mazingira ya mabadiliko ya dunia ya leo. Tunapoiachilia dhana ya kuiga mfano mwema kutoka kwenye mipaka ya mbinu za kihistoria, na kuweka roho ya kushikamana na uongozi wa kidini, utulivu wa kiroho, kutafuta baraka, haya na kujitolea kuwa msingi wa mahusiano ya kifamilia, nyumba hugeuka kuwa mahali salama ambapo uchovu wa dunia ya leo yenye kelele na misukosuko huyeyuka. Katika mazingira hayo, kizazi kijacho hukua na kustawi kikiwa na usalama wa kisaikolojia na heshima inayotokana na imani.
-
Khutba ya Sala ya Ijumaa Jamiat Al-Mustafa Mbezi Beach: Nafasi ya Baadhi ya Wanazuoni wa Dini wa Leo katika Kupotosha Mafundisho ya Kidini
Imam wa Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Jamiat Al-Mustafa (saw), Mbezi Beach – Dar es Salaam, Tanzania, amezungumzia nafasi ya baadhi ya wanazuoni wa dini wa zama hizi katika kupotosha na kuondoka katika mafundisho sahihi ya dini, akisisitiza umuhimu wa kurejea katika Qur’ani Tukufu, Hadithi sahihi, misingi ya kielimu na maadili ya Kiislamu katika kufafanua mafundisho ya dini.
-
Ayatollah Mojtaba Khamenei: Kuchochea Mfarakano Baina ya Waislamu Hakukubaliki Tena
Ayatollah Sayyid Mojtaba Khamenei amesema kuwa katika zama hizi si sahihi tena kuhusisha uchochezi wa mfarakano baina ya Waislamu na ujinga au uzembe, wakati madhalimu wa dunia, wakiongozwa na Marekani, wameweka wazi malengo yao ya kikoloni na mipango ya kutawala na kuonyesha wazi nia zao za kuleta madhara.
-
Wanahabari ni Wasimuliaji wa Ukweli na Mashahidi wa Zama
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRNA), Hussein Jaberi Ansari, ametembelea mji wa Borujerd katika maadhimisho ya Siku ya Wanahabari nchini Iran, akisisitiza umuhimu wa wanahabari kama wasimuliaji wa ukweli na mashahidi wa matukio ya zama zao.