2 Septemba 2026 - 21:08
Ayatollah Mojtaba Khamenei: Kuchochea Mfarakano Baina ya Waislamu Hakukubaliki Tena

Ayatollah Sayyid Mojtaba Khamenei amesema kuwa katika zama hizi si sahihi tena kuhusisha uchochezi wa mfarakano baina ya Waislamu na ujinga au uzembe, wakati madhalimu wa dunia, wakiongozwa na Marekani, wameweka wazi malengo yao ya kikoloni na mipango ya kutawala na kuonyesha wazi nia zao za kuleta madhara.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Ayatollah Sayyid Mojtaba Khamenei amesema kuwa katika zama hizi, si jambo linalokubalika tena kwa mtu kuhusisha vitendo vya kuchochea mfarakano baina ya Waislamu na ujinga au uzembe.

Akizungumza katika ujumbe wake wa tarehe 30 Agosti 2026, Ayatullah Mojtaba Khamenei amehoji namna mtu anavyoweza kudai kuwa hajui au ametenda kwa uzembe katika kuchochea migogoro na mfarakano miongoni mwa Waislamu, wakati hali ya dunia imekuwa wazi zaidi.

Amesema madhalimu wa dunia, akiwemo Marekani, wameondoa pazia za udanganyifu zilizokuwa zikificha malengo yao ya kikoloni na mipango yao ya kutawala na kujitwalia mamlaka juu ya mataifa mengine.

Kwa mujibu wa Ayatullah Mojtaba Khamenei, madhalimu hao wameacha pia mbinu zao za kujisitiri na sasa wameonyesha wazi misimamo na malengo yao mbele ya ulimwengu.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa Waislamu kuwa na uelewa katika mazingira haya na kutoruhusu vitendo vinavyoweza kuchochea migawanyiko na migogoro miongoni mwao.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha