wapinzani
-
Mhadhiri wa Masomo ya Ngazi ya Juu katika Hawza ya Qom asisitiza:
Lengo kuu la utawala wa Amirul-Mu’minin (a.s) ni kuwaongoza wanadamu / mpaka kati ya uhuru wa kujieleza na vitendo dhidi ya usalama wa umma
Mheshimiwa Sayyid Mujtaba Nourmofidi, Rais wa Taasisi ya Utafiti wa Fiqhi ya Kisasa, alipohudhuria Shirika la Habari la ABNA, alichambua mada ya: “Fiqhi ya kisiasa katika kuweka mipaka kati ya uhuru wa kujieleza na ukosoaji halali, dhidi ya uasi na vitendo vinavyohatarisha usalama wa umma katika utawala wa Imam Ali (a.s)”.
-
Mtaalamu wa masuala ya usalama: Kikosi cha mtandaoni (cyber) cha Taliban kinafanya shughuli zake kuanzia Ulaya hadi Marekani dhidi ya wakosoaji wao
Bismillah Taban, mtaalamu wa masuala ya usalama kutoka Afghanistan, anasema kuwa Taliban kwa kutumia akaunti bandia na zilizoandaliwa kwa uratibu katika maeneo mbalimbali ya saa duniani, wameanzisha vita vya kimfumo vya kuwachafua wapinzani wao, hasa wakosoaji wa Kishia na vyombo vya habari huru; mbinu ambayo kwa mtazamo wa wachambuzi ni mwendelezo wa sera ya ukandamizaji wa Taliban katika uwanja wa maoni ya umma.
-
Je, Taurati imebadilishwa? Angalia jibu la Qur’an hapa!
Kuhusu taarifa (maelezo) ya Qur’an Tukufu kuhusu ubadilishaji wa maneno ya Taurati, kuna mjadala wa kiitihadi kama ifuatavyo: 1. Mtazamo maarufu (ushahidi unaoonekana wazi kabisa katika Quran) Watafiti wengi na wafuasi wa mtazamo huu wanaona kwamba Qur’an inazungumzia ubadilishaji wa maneno kwa uwazi jabisa. Qur’an inataja maneno yaliyopinduliwa au kuharibiwa na baadhi ya Watu wa Kitabu (Ahlul-kita'bi): «يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَوَاضِعِهِ» (An-Nisa 46) Hapa (kwa mujibu wa Aya hiyo Tukufu) , ubadilishaji huo unahusiana na maneno yenyewe, na si tafsiri tu. 2. Mtazamo wa wapinzani (Mukhalifuna) Wao wanasema kuwa Qur’an inazungumzia ubadilishaji wa maana, si maneno ya kifasihi: Wanasema kuwa maneno ya msingi hayajabadilishwa, lakini maana au tafsiri potofu ndizo zilizobadilishwa au kutumika vibaya. Hii inaitwa ubadilishaji wa maana (tafsiri) badala ya ubadilishaji wa maneno.
-
Barua za Nahjul Balagha - Barua ya 32 | Mbinu za Muawiya, Njia ya Vyombo vya Habari vya Kigeni vya Leo
Mbinu za vyombo vya habari katika kueneza batili na kuunda shubha ili kuwazamisha watu ndani ya fikra zisizo za Kimungu zimekuwa zikitumiwa na wapinzani wa njia ya haki katika vipindi vyote vya historia. Ingawa njia hizi hubadilika kulingana na zama, malengo yao hubaki yale yale. Kurejea mbinu hizi katika mojawapo ya barua za Imam Ali (a.s) kwa Muawiya na kulinganisha na mbinu za vyombo vya habari vya kigeni katika ulimwengu wa leo kunadhihirisha ukweli kwamba “Muawiya na wanaofanana naye” katika historia wamejitahidi kupotosha wengine ili kufikia malengo yao wenyewe-juhudi ambazo hatimaye hupelekea maangamizi yao pamoja na maangamizi ya wale wanaowafuata.
-
Muonekano wa Hali ya Kitamaduni na Kielimu ya Ardhi ya Gaza / Sehemu ya Kwanza: Kutoka kwa Familia za Kielimu na Kitamaduni Hadi Wairani Walioko Gaza
Ardhi ya Gaza, eneo lenye historia ya zaidi ya miaka elfu nne ya makazi ya binadamu, linatambulika kama mojawapo ya vituo muhimu vya ustaarabu Kusini-Mashariki mwa Asia. Ingawa katika karne moja iliyopita, uhalifu wa serikali ya kikoloni ya Kiingereza na utawala wa uongo wa Kizayuni umeharibu ishara nyingi za kitamaduni na ustaarabu wa eneo hili, vyanzo vya kihistoria vinaonyesha ishara nyingi za historia hii ya kupendeza.
-
Utawala wa Saudi umemnyonga kijana mmoja wa Shi’a kutoka Qatif
Wapinzani wa Saudi wameeleza kuwa Mohammed Al-Ammar hakuwa mtenda dhambi wala mwanamgambo; bali alikuwa kijana aliyeota uhuru, heshima, na haki za kijamii. Lakini utawala ambao haukubali mazungumzo, unapandisha mti wa kifo mbele ya sauti ya uhuru, na hukata vichwa dhidi ya yale yanayodaiwa kwa amani.
-
Mashambulizi ya Kipuuzi Zaidi Kufuatia Kuongezeka kwa Umaarufu na Ushindi wa Mamdani katika Uchaguzi wa Awali wa Umeya wa New York
Zahran Mamdani, Mbunge wa jimbo na mgombea wa chama cha Demokratik katika uchaguzi wa Umeya wa New York, kupitia kampeni za wananchi amefanikiwa kuwashinda wapinzani maarufu kama Andrew Cuomo katika kinyang’anyiro cha awali na kuwa mgombea wa kwanza Mwislamu kwa nafasi hiyo. Ushindi huo, hata hivyo, umekumbwa na mashambulizi ya chuki na matusi ya Uislamu kutoka kwa baadhi ya wanasiasa, lakini yeye pamoja na wafuasi wake wametangaza kuwa hawatarudi nyuma mbele ya chuki na ubaguzi.
-
Mkutano wa wapinzani wa kisiasa wa Taliban nchini Pakistan: Kuunda serikali ya pamoja kutasaidia amani na utulivu wa Afghanistan
Mkutano wa baadhi ya wapinzani wa kisiasa wa serikali ya Taliban ukiwa na kaulimbiu ya “Kuelekea Umoja na Uaminifu” umefanyika kwa siku mbili mjini Islamabad, mji mkuu wa Pakistan. Katika mkutano huu, baadhi ya wasichana wa Shia, wakiwemo Zahra Joyaa, mwanahabari maarufu kutoka Afghanistan, pia walihudhuria.