Main Title

source :
Jumatano

2 Oktoba 2024

20:04:50
1491051

Wakazi wa Tehran wakusanyika kuunga mkono mashambulio ya makombora dhidi ya Israel

Wananchi wa mji mkuu wa Iran Tehran leo wamekusanyika katika medani ya Imam Hussein (as) na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa Operesheni ya Ahadi ya Kweli-2 ya mashambulio ya makombora ya Iran dhidi ya utawala haramu wa Israel.

source :
Jumatano

2 Oktoba 2024

20:04:18
1491050

Araghchi: Tumejiandaa kwa mashambulio tarajio ya Israel, jibu letu litakalofuata litakuwa kali zaidi

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kuwa, operesheni ya makombora ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) dhidi ya maeneo ya utawala wa Kizayuni wa Israel yalikuwa ni ya kujihami kikamilifu na kusisitiza kuwa: Iwapo utawala wa Kizayuni utataka kujibu mashambulio hayo, basi jibu letu litakalofuata litakuwa kali zaidi.

source :
Jumatano

2 Oktoba 2024

20:03:50
1491049

Spika wa Bunge: Tumewaonyesha wavamizi sehemu ndogo tu ya uwezo wa Iran

Mohammad Baqir Qalibaf, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza operesheni ya makombora ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH dhidi ya utawala wa Kizayuni na kusisitiza kuwa, wavamizi wameonyeshwa sehemu ndogo tu nguvu ya Iran.

source :
Jumatano

2 Oktoba 2024

20:03:27
1491048

Rais Pezeshkian: Wazayuni wakithubutu kufanya kosa, watapata jibu kali zaidi la Iran

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kwamba operesheni ya makombora ya jana ya kujivunia ya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya Israel kwa mara nyingine tena imethibitisha kwamba ngao ya chuma inayodaiwa Wazayuni ni dhaifu kuliko kioo.

source :
Jumatano

2 Oktoba 2024

20:02:56
1491047

Operesheni ya Ahadi ya Kweli-2: Hatua ya Iran ya kujilinda kihalali

Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelitaja shambulio kali la makombora la Iran la Oktoba Mosi dhidi ya utawala haramu wa Israel kuwa ni haki yake halali ya kujilinda kwa msingi wa Kifungu cha 51 cha Hati ya Umoja wa Mataifa.

source :
Jumatano

2 Oktoba 2024

18:55:42
1491000

Mufti Mkuu wa Russia ametoa pole kwa kifo cha kishahidi cha Syed Hassan Nasrullah

Mkuu wa idara ya kidini ya Waislamu wa Shirikisho la Urusi na Mufti Mkuu wa nchi hii ametoa salamu za rambirambi kutokana na kuuawa Shahid Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon.

source :
Jumatano

2 Oktoba 2024

13:16:49
1490876

Kichwa cha Habari cha gazeti rasmi la Iraq: "Makombora ya Iran yauchoma moto utawala wa Kizayuni"

Kichwa cha habari cha gazeti la Iraq, "Al-Sabah", gazeti rasmi la nchi hii, kilipewa jina hili: "Roketi za Iran zauchoma moto utawala wa Kizayuni".

source :
Jumatano

2 Oktoba 2024

13:15:33
1490874

Baraza la Makanisa la Mashariki ya Kati limedai na kuzitaka jumuiya za kimataifa kuchukua hatua ya kusitisha mashambulizi dhidi ya Lebanon.

Katika taarifa yake, Baraza la Makanisa la Mashariki ya Kati limelaani mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Lebanon na kupuuza Sheria za Kimataifa na Mikataba ya Geneva.

source :
Jumatano

2 Oktoba 2024

13:14:06
1490872

Siri za kula kiafya katika mafundisho ya Kiislamu

Lishe bora ni moja ya mambo muhimu katika kudumisha afya ya mwili na roho katika mafundisho ya dini. Uislamu unaelekeza umuhimu maalum kwa ulaji wa kiafya kwa kutoa miongozo ya kina kuhusu kuchagua aina ya chakula, jinsi ya kukitumia na kuzingatia kula kwa kiasi. Kanuni hizi husaidia si tu katika kupona kimwili, bali pia katika ukuaji wa kiroho.

source :
Jumatano

2 Oktoba 2024

11:16:58
1490819

Ripoti ya Video | Picha ya ukumbusho ya ripota wa Kipalestina huko Gaza akiwa na makombora ya Iran

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - "Ismail Al-Dahdouh" Mwandishi wa Habari wa Kipalestina alichukua / alipiga picha ya ukumbusho huko Gaza kwenye makombora yaliyorushwa kutoka katika ardhi ya Iran kuelekea maeneo yanayokaliwa kwa mabavu (na utawala Haram wa Israel).

source :
Jumatano

2 Oktoba 2024

01:49:00
1490655

Video | Makombora ya Balistiki ya Iran yalenga shabaha zake moja kwa moja kwenye ardhi zinazokaliwa kimabavu

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Kulingana na video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, makumi ya makombora ya Balistiki ya Iran yalipenya mifumo ya ulinzi wa anga ya utawala haram wa Kizayuni na kugonga moja kwa moja kwenye shabaha zilizokusudi kwa usahihi zaidi katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu na Israel.

source :
Jumanne

1 Oktoba 2024

16:00:07
1490471

Tume ya Haki za Binadamu ya Kiislamu ya Uingereza: Mauaji ya Katibu Mkuu wa Hizbullah ni ushahidi wa mauaji ya kimbari ya Israel

Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Kiislamu ya Uingereza (IHRC) amesema kuwa, jinai za kivita za hivi karibuni za utawala ghasibu wa Israel katika mauaji ya Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon na kuuawa mamia ya watu katika shambulio la Beirut ni ushahidi wa wazi wa mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni.

source :
Jumanne

1 Oktoba 2024

15:59:39
1490470

HAMAS: Tumeangamiza idadi kubwa ya askari wa Israel Gaza

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza habari ya kuangamiza idadi kubwa ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kusini mwa Ukanda wa Gaza.

source :
Jumanne

1 Oktoba 2024

15:59:17
1490469

Radiamali ya Nicaragua kwa mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni huko Palestina na Lebanon

Valdrack Jaentschke Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Nicaragua amekosoa vikali na mfumo usio wa haki unaotawala dunia hivi sasa na kulaani vikali mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni na waitifaki wake dhidi ya watu madhulumu wa Palestina na Lebanon.

source :
Jumanne

1 Oktoba 2024

15:58:48
1490468

Israel yashambulia kwa mabomu makazi ya wakimbizi wa Kipalestina Gaza

Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zimeshambulia kwa mabomu shule ya makazi ya Wapalestina katika mji wa Gaza.

source :
Jumanne

1 Oktoba 2024

15:58:20
1490467

UNICEF yaeleza wasiwasi wake kuhusu hali mbaya ya watoto wa Lebanon

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, ametahadharisha kuhusu hali mbaya ya kibinadamu nchini Lebanon na ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya watoto nchini humo.

source :
Jumanne

1 Oktoba 2024

15:57:50
1490466

Hizbullah ya Lebanon yawatwanga tena kwa makombora wanajeshi wa utawala wa Kizayuni

Wanamapambano wa Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon wamefanya mashambulizi mengine makali kwa kulitwanga kwa makombora eneo walipokuwa wamekusanyika wanajeshi wa utawala wa Kizayuni katika maeneo ya kaskazini mwa ardhi za Palestina zinayokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel.

source :
Jumanne

1 Oktoba 2024

15:57:20
1490465

Rais wa Iran akosoa undumakuwili wa Marekani na Ulaya kuhusu haki za binadamu

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa undumakuwili wa Marekani na madola ya Ulaya kuuhusiana na haki za binadamuu na kusema, kimya cha nchi za magharibi mbele ya mauaji ya maelfu ya watu wasio na hatia ni kugonga muhuri wa kuunga mkono jinai hizi.

source :
Jumanne

1 Oktoba 2024

15:56:51
1490464

Kukosoa Araghchi "kutochukua hatua" Baraza la Usalama kukabiliana na jinai za Wazayuni dhidi ya Gaza na Lebanon

Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameitaja hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kutochukua hatua kutokana na ukwamishaji mambo wa Marekani na waungaji mkono wengine wa Magharibi wa Israel kuwa ndio sababu kuu ya kuendelea jinai, chokochoko na vitendo visivyo halali vya utawala haramu wa Kizayuni.

source :
Jumanne

1 Oktoba 2024

15:56:17
1490463

Rais wa Iran kuelekea Qatar kesho Jumatano

Rais wa Iran kesho Jumatano ataondoka hapa Tehran na kuelekea Qatar kwa madhumuni ya kushiriki katika kikao rasmi wa nchi mbili na kushiriki katika Jukwaa la Mazungumzo ya Ushirikiano wa Asia.