7 Oktoba 2021 - 14:02
Imethibitishwa kuwa rais mtoro wa Afghanistan aliiba mamilioni ya dola alipokimbilia nje ya nchi

Msemaji wa kundi la Taliban Zabihullah Mujahid amethibitisha kuwa Muhammad Ashraf Ghani, rais mtoro wa Afghanistan aliiba na kuondoka na mamilioni ya dola wakati alipokimbilia nje ya nchi.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Pasi na kuashiria kiwango halisi cha fedha hizo, msemaji wa Taliban amesema, Muhammad Ashraf Ghani aliiba fedha hizo wakati alipotoroka Afghanistan.

Zabihullah Mujahid ameongeza kuwa, Ikulu ya rais wa Afghanistan imelipatia kundi la Taliban taswira zinazowaonyesha wafanyakazi wa Ikulu hiyo wakipigana na kusokotana kwa ajili ya kugombania fedha zilizosalia.

Kabla ya kauli hiyo ya msemaji wa Taliban vyombo kadhaa vya habari vilishawahi kuripoti kuwa, Ashrafi Ghani aliiba mamilioni ya dola za Kimarekani wakati alipotoroka nchi, lakini Ghani mwenyewe alikanusha madai hayo.

Tarehe 15 Agosti, vikosi vya kundi la Taliban viliingia mji mkuu wa Afghanistan Kabul; na sambamba na kuingia vikosi hivyo mjini humo, rais Ashraf Ghani aliitoroka nchi; na hivi sasa amepatiwa hifadhi ya kisiasa katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).../


342/