Sisitizo hilo limetolewa mara baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kutangaza pendekezo jipya la kusitisha vita ambalo amesema limeidhinishwa na Israel na kuitaka harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ilikubali. Ofisi ya Netanyahu imeendelea kusema: "vita havitakwisha hadi malengo yake yote yafikiwe, ikiwa ni pamoja na kurejea kwa mateka wetu wote na kuangamizwa uwezo wa kijeshi na kiutawala wa Hamas." Hata hivyo taarifa ya ofisi hiyo imeongeza kuwa, Netanyahu ameipa idhini timu ya mazungumzo ya Israel "kuwasilisha muongozo wa kufikia lengo hilo," akimaanisha kukombolewa mateka.Pendekezo hilo lililotangazwa na Biden, litatekelezwa kwa awamu tatu, ya kwanza ikichukua wiki sita na kujumuisha usitishaji vita kamili, kuondolewa vikosi vya jeshi la Kizayuni kutoka maeneo yenye watu wengi huko Ghaza, na kubadilishana mateka.
342/