9 Mei 2025 - 14:42
Ikwiriri - Tanzania | Swala ya Alfajiri na Ibada zinazofuatia hususan Dua ya Nudba ambayo husomwa zaidi siku za Ijumaa na siku maalum kama vile Eid

Dua ya Nudba ni dua maarufu inayosomwa hasa Siku za Ijumaa na Siku maalum kama vile Siku za Eid, na katika nyakati za kutaka kumbukumbu ya Imam Mahdi (a.t.f.s). Dua hii adhimu, inaonyesha huzuni na hamu ya kukutana na Imam wa Zama (a.t.f.s), na inawasifu Ahlul-Bayt(as) wa Mtume Muhammad(s.a.w.w).

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Swala ya Asubuhi na Ibada Zinazofuatia hususan Dua ya Nudba katika kila Siku ya Ijumaa - Husomwa mara kwa mara katika Hawza ya Imam Reza (as), Ikwiriri - Tanzania, na ni kama ifuatavyo:

Ikwiriri - Tanzania | Swala ya Alfajiri na Ibada zinazofuatia hususan Dua ya Nudba ambayo husomwa zaidi siku za Ijumaa na siku maalum kama vile Eid

1. Swala ya Asubuhi (صلاة الصبح):
Swala ya alfajiri kama inavyotambulika na kufahamika ni Swala ya kwanza ya Siku, na ina rakaa mbili. Hii ni ibada muhimu sana kwa kila Muislamu. Inaswaliwa baada ya adhana ya alfajiri, na kabla ya jua kuchomoza.

2. Dua ya Nudba (دعاء الندبة):
Dua ya Nudba ni dua maarufu inayosomwa hasa Siku za Ijumaa na Siku maalum kama vile Siku za Eid, na katika nyakati za kutaka kumbukumbu ya Imam Mahdi (a.t.f.s). Dua hii adhimu, inaonyesha huzuni na hamu ya kukutana na Imam wa Zama (a.t.f.s), na inawasifu Ahlul-Bayt(as) wa Mtume Muhammad(s.a.w.w).

3. Ta'qibat baada ya Swala:
Baada ya kuswali, kuna dua na tasbih mbalimbali zinazopendekezwa, kama vile:

Tasbih ya Bi.Fatima (a.s): 34 × Allahu Akbar, 33 × Alhamdulillah, 33 × Subhanallah

Ikwiriri - Tanzania | Swala ya Alfajiri na Ibada zinazofuatia hususan Dua ya Nudba ambayo husomwa zaidi siku za Ijumaa na siku maalum kama vile Eid

Istighfar

Kusoma Ayat al-Kursi na surat Qul-huwa Allahu Ahad, Falaq, na Nas.

4. Ibada hizi na Dua hii maalum ya Nudba, husomwa kila Siku ya Ijumaa katika Taasisi ya Hojjatul Asr Socierty of Tanzania - Katika Hawza ya Imam Ridha (as):
Taasisi hii, inakusanya vijana au wanafunzi wa Kiislamu, wanaosoma katika Hawza ya Imam Ridha (a.s), iliyopo chini ya Usimamizi wa Samahat Sayyid Aref Naqvi, na hii ni moja ya Hawza za Kidini zinazotoa mchango mkubwa katika kukuza elimu na maadili ya Kiislamu.

Maelezo ya Jumla:

Katika Hawza Imam Ridha (a.s.), kunaendelea ndani yake ibada mbalimbali na ratiba muhimu za kujifunza maarifa ya Dini Tukufu ya Kiislamu. Tunawaombea Wanafunzi wa Hawza hii: Baraka , Taufiq, na Mafanikio katika safari yao ya kiroho na kielimu.

Ikwiriri - Tanzania | Swala ya Alfajiri na Ibada zinazofuatia hususan Dua ya Nudba ambayo husomwa zaidi siku za Ijumaa na siku maalum kama vile Eid

Your Comment

You are replying to: .
captcha