Mtandao wa Kimataifa wa Kiyahudi wa Kupambana na Wazayuni, (The International Jewish Anti-Zionist Network) ambao unasema wanachama wake ni wa Kiyahudi, umetangaza kuwa zaidi ya watu100 walishiriki katika maandamano hayo. Kundi hilo lilifunua mabango kwenye ukumbi wa ubalozi huo mdogo wa Israel baada ya kuuvamia, ikiwa ni pamoja na lenye maandishi yanayosomeka: “kufanya mauaji ya kimbari huwafanya Wayahudi wawe na usalama mdogo zaidi; si kwa jina langu!”Mmoja wa waandamanaji aitwaye Sarah mwenye umri wa miaka 54 amesema: "tunafanya hivi kwa sababu sisi ni sehemu ya umati unaoongezeka wa watu wanaotaka kukomeshwa mauaji ya kimbari na ambao wako katika mshikamano na Palestina na wana wasiwasi sana kuhusu ushiriki wa serikali ya Marekani katika mauaji ya kimbari yanayotokea".
Zaidi ya Wapalestina 36,470, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wameshauawa hadi sasa katika vita vya kinyama na mauaji ya kimbari yaliyoanzishwa na jeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza kufuatia operesheni ya kulipiza kisasi ya Kimbunga cha Al-Aqsa iliyotekelezwa na harakati za Muqawama wa Palestina za Ghaza Oktoba 7,2023
Tangu vilipoanza vita hivyo, Marekani imekuwa ikiusaidia na kuuunga mkono utawala wa Kizayuni kwa kuupatia maelfu ya tani za silaha na zana za kijeshi ambazo unazitumia kuteketezea roho za Wapalestina wasio na ulinzi.../
342/