Miaka thelathini na sita iliyopita Julai 2, 1988, abiria wote 290, waliokuwa ndani ya ndege ya abiria ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wakiwemo watoto 66 na wanawake 53, waliuawa shahidi wakati meli ya kivita ya Marekani Vincennes ilipoitungua kwa kombora ndege hiyo.
Kuhusu ugaidi huo wa wazi, Ali Bagheri Kani Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ameandika katika mtandao wa kijamii wa X, akiashiria kupita zaidi ya miaka thelathini na sita tangu kutekelezwa kitendo hicho cha woga na kigaidi cha Marekani kulenga ndege ya abiria ya Iran katika anga ya Ghuba ya Uajemi na kusema ukiukaji huo wa wazi wa Magharibi dhidi ya haki za binadamu za watu wa Iran ungali unaendelea kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwekewa vikwazo vya kidhalimu.
Ali Bagheri Kani, aidha ameongeza kwa kusema kuwa uungaji mkono mkubwa wa Marekani kwa jinai za utawala unaokalia kwa mabavu Palestina ni jinai nyingine katika historia ndefu ya umwagaji damu ya watawala wa Marekani katika kutekeleza mauaji ya kizazi, mauaji ya halaiki, kusababisha njaa, uporaji ardhi na uharibifu. Huku akiashiria kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesimama kidete katika kukabiliana na jinai hizo licha ya mashinikizo yote yanayotolewa dhidi yake kimataifa, Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema uingiliaji haramu unaofanywa na Marekani katika maeneo tofauti ya dunia umeifanya nchi hiyo kuwa mmoja wa wavunjaji wakuu wa haki za binadamu duniani. Bagheri Kani amefafanua kwamba hatua za upande mmoja na utumiaji wa vikwazo na uungaji mkono wa pande zote na usio na masharti wa Marekani kwa mauaji ya kimbari na jinai za utawala wa Kizayuni ni miongoni mwa hatua mbaya zaidi dhidi ya haki za binadamu ambazo Marekani imezifanya hadi sasa na inaendelea kuzifanya. Bagheri Kani ameongeza kuwa leo hii ulimwengu wote unashuhudia maana halisi ya haki za binadamu kwa mtazamo wa Marekani na utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza.
342/